Advertisements

Sunday, August 28, 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Linda Thomas-Greenfield walipokutana wakati wa Mkutano wa TICAD VI Jijini Nairobi na kuzugumzia masuala ya ushirikiano. Wakati wa mazungumzo hayo Mhe. Dkt. Kolimba alimshukuru Mhe. Greenfield kwa ushiriano uliopo kati ya Tanzania na Marekani ambapo nchi hiyo imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kuboresha huduma za afya na miradi mingine ya maendeleo. 
Mhe. Naibu Waziri akizungumza na Mhe. Greenfield 
Mazungumzo yakiendelea kati ya Mhe. Dkt. Susan na Mhe. Greenfield (hayupo pichani). Wengine katika picha ni Bi. Talha Waziri (kushoto), Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Bi. Bertha Makilagi (kulia), Afisa Mambo ya Nje. 
Mhe. Greenfield akiwa na ujumbe wake nae akichangia jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Dkt. Susan (hayupo pichani) 
Mhe. Dkt. Susan aiagana na mgeni wake Mhe. Greenfield mara baada ya mazungumzo huku Bi. Makilagi (katikati) akishuhudia 
Mhe. Naibu Waziri (mwenye gauni la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi Talha Waziri (wa pili kutoka kulia), Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri na Bi. Bertha Makilagi (kushoto), Afisa Mambo ya Nje. 

No comments: