Advertisements

Friday, August 12, 2016

TANZANIA KUKABIDHIWA UENYEKITI WA SADC-TROIKA, NCHINI SWAZILAND

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Mkutano uliofanyika Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Agosti, 2016. Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alizungumza kuhusu maazimio ya Mkutano wa 17 wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (Double Troika) uliofanyika Maputo nchini Msumbiji tarehe 7 Julai, 2016. Maazimio hayo ambayo pamoja na mambo mengine ni kuhusu hali ya amani na usalama katika nchi za kanda hiyo, yatawasilishwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaotarajiwa kufanyika tarehe 31 Agosti, 2016 nchini Swaziland ambapoTanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya Mwenyekiti katika Asasi hiyo.

Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent Shiyo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga.

No comments: