Advertisements

Tuesday, August 16, 2016

VIONGOZI WA YANGA WALIOVULIWA UANACHAMA NA MANJI WATINGA TFF

Wiki kadhaa baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kuwavua uanachama baadhi ya wajumbe wa klabu hiyo, viongozi ha walivuliwa uanachama wamepeleka barua ya kupinga kuvuliwa uanachama katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Hilo yamesemwa Msemaji wa TFF, Alfred Lucas wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema barua hiyo iliwasilishwa katika shirikisho hilo Agosti 12, 2016.
“Kuna wanachama wakiokuwa viongozi wa Yanga waliotimuliwa uanachama Agosti 6, mwaka huu walileta barua ya malalamiko TFF, ” amesema Lucas.
Ameongeza kuwa “nathibitisha kuwa malalamiko yao yamepokelewa ambayo yanalenga kutaka haki itendeke.”
Amesema barua hiyo inasema kuwa uongozi wa Yanga ulikiuka taratibu na katiba ya klabu hiyo ilipowafuta uanachama.
“TFF imeyapokea malalamiko hayo na yatapelekwa katika kamati husika pindi yatakapofanyiwa maamuzi tutawajulisha wadau wa mpira wa miguu nchini,” amesema.
Wanachama waliovuliwa uanachama ni pamoja na Ayubu Nyenzi na Hashim Abdallah.

No comments: