Advertisements

Wednesday, September 28, 2016

TRA WAIBUKA VINARA WA UTOAJI TAARIFA KWA UMMA MWAKA 2016

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer akizungumza na wadau wa habari kwenye maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Haki za Kupata Taarifa Septemba 28 KATIKA ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameibuka washindi wa TUZO ya UFUNGUO WA DHAHABU kwa kuwa taasisi inayofunguka zaidi kwa wananchi hapa Tanzania kwa mwaka 2016. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika hoteli yaa Sea Shells hapa Dar es Salaam.
Katika tuzo hizo Wizara ya Sheria na Katiba imeambulia Kufuli la Dhahabu kwa kuwa taasisi ngumu kwa upatikanaji wa taarifa kwa Umma.

MISA Tanzania pia walizindua Ripoti ya kila mwaka ya Upatikanaji Taarifa katika Taasisi za Umma kwa mwaka 2016.

Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa habari kuhusu vigezo vilivyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) katika katika Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.

Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi kutoka Arusha, Mussa Juma akichangia mada kuhusu utoaji wa taarifa kwa umma 
Afia Habari kutoka UNESCO, Christopher Regay akichangia mada wakati wa  Taasisi ya MISA Tanzania kutoa taarifa njia kufanya utafiti kwa taasisi mablimbali zinazotoa taarifa kwa umma Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
 Meneja Viwango na Udhibiti wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike akichangia mada pamoja na kujibu hoja za waandishi wa habari waliofika katika Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club, Modesti Jerome Nkwilu akizungumza jambo wakati wa utoaji wa tuzo za utoaji wa taarifa kwa umma zilizotolewa na MISA Tanzania katika Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
Mwenyekiti wa Club ya Waandishi wa Habari mkoa wa Singida, Ranko Banadi akichangia mada wakati wa utoaji wa taarifa kwa umma.
Mwenyekiti wa Kilimanjaro Press Club, Bahath Nyakiraria akizungumza jambo wakati wa utoaji wa tuzo za utoaji wa taarifa kwa umma zilizotolewa na MISA Tanzania katika Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa chapicho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini katika Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer( wa pili kutoka kulia) na Afisa Habari na Utafiti wa Misa-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa( wa pili kutoka kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wakiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kitabu cha ripoti ya haki ya kupata taarifa halali katika sekta za umma katika Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer akiwazungumza jambo na Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa baada ta tuzo ya Kufuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2016 lililokwenda kwenye Wizara ya Sheria na Katiba
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Makao, Gabriel Mwangosi baada ya kutwa tuzo ya TRA katika utoaji wa taarifa kwa umma
Meneja wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Makao, Gabriel Mwangosi  akipewa pongezi na Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa baada ya kupokea tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa utoaji taarifa kwa umma.
kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa jana jijini Dar es Salaam 
Meneja wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Makao, Gabriel Mwangosi  akionesha tuzo ya ufunguo wa dhahabu kwa waandishi wa habari mara baada ya Mamlaka ta Mapato Tanzania(TRA) kuibuka mshindi wa kwanza wa kutoa taarifa kwa umma
Baadhi ya wadau wa habari nchini wakiendelea kufuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.

1 comment:

Anonymous said...

Download New Audio | Aslay - Kidawa >>> https://goo.gl/hkCv5c