Advertisements

Monday, October 3, 2016

KUNDI LA MWANAGATI YETU WATAMBULISHANA NA KULA BATA LA NGUVU GOLDEN PARIS PUB DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Mwanagati Yetu Group Bw Harold Urio akisoma hotuba katika sherehe ya kuwakutanisha na kufahamiana kwa wanakikundi hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Golden Paris Pub Mwanagati Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, Sherehe hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mgeni mwalikwa katika sherehe hiyo Diwani wa Kata ya Mzinga Ndugu Job Isack akitoa nasaha zake kwa wanakikundi wa Mwanagati Yetu.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwanagati Ndugu Chacha Momba akizungumza katika sherehe hiyo kulia ni Injinia Josephat Kyando aliyekuwa MC wa Sherehe hiyo na mtunza hazina wa kamati ya sherehe.
Injinia Cyprian Luhemeja ambaye pia alikuwa mgeni mwalikwa akitoa nasaha zake kulia ni Injinia Kyando.
Mwendeshaji wa kundi la Mwanagati Yetu Group Bw. Awene Nsolo akijitambulisha mbele ya wanakikundi.
Wageni wakipata chakula.
Viongozi wa kundi wakipata chakula kutoka kulia ni Godwin Kaaya, Jackton Ochieng na Awene Nsolo.
Mmoja wa wanakikundi Bw. Geofrey Tengeneza akijitambulisha kwa wanakikundi wenzake.
Bwana Imani Lwinga aka Serengeti akijitambulisha pia.
Viongozai na kamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya wanakikundi wakijadiliana jambo wakati wa sherehe hiyo.

No comments: