Advertisements

Monday, October 3, 2016

MAKONDA AUNGURUMA BUGURUNI

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya Jumapili Octoba 2, 2016 katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ili kuzungumzia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. 

Katika Mkutano huo Makonda amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza au kuondoa kabisa changamoto zinazowakabili ikiwemo, vibaka, dadapoa na uchafu wa mazingira, akisema, ikiwa wananchi watashitiki kikamilifu ni rahisi kukomesha tatizo la vibaka kwa sababu vibaka na dadapoa wanatoka miongoni mwa familia zao na hali kadhalika uchafu wa mazingira unatokana na takataka wanazozalisha wananchi wenyewe.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, PaulMakonda wakati akiwahutubia jioni ya Jumapili Octoba 2, 2016 katika neo la Buguruni kwa Mnayamani
Viongozi waandamizi katika Wilaya ya Ilala, wakimsikiliza mkuu wa mkoa Paul Makonda wakati akihutubia wananchi katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela, Ofisa Tawala wa Manispaa hiyo, Edward Mpogolo, Naibu Meya Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Segerea wilayani humo Bona Kalua
Mjumbe wa Shina namba tano, Katika Kata ya Myamani, Buguruni Zubeda Lugiga, akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara.
Mkazi wa Buguruni, Sadik Mgaya akieleza changamoto na kero zinazowakabili wananchi wa eneo hilo wakati wa mkutano huo wa Makonda
Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Samweli Ndyanabo, akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara siku ya Jumapili 
jioni  
Octoba 2, 2016 
Kamanda wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), uliofayika 
siku ya Jumapili jioni  Octoba 2, 2016 
Buguruni kwa Mnyamani
Kamanda wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uliofayika 
siku ya Jumapili jioni  Octoba 2, 2016 
 Buguruni kwa Mnyamani 
Wananchi wakishangilia wakati hoja zao zikijibiwa na Kamanda Sillo
Wananchi wakishangilia wakati hoja zao zikijibiwa na Kamanda Sillo 
Ofisa tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, akimsikiliza kwa karibu Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema, aliyekuwa akielezea jambo,wakati wa mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika 
siku ya Jumapili jioni  Octoba 2, 2016 
Buguruni kwa Mnyamani Dar es Salaam. Katikati ni Mbunge wa Segerea Bona Kalua 
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akitoa maelezo yake kuhusu maswali waliyouliza wananchi, wakati wa mkutano wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, paul Makonda uliofanyika 
siku ya Jumapili jioni  Octoba 2, 2016 
. Naibu Meya huyo alizungumzia zaidi mradi wa Uwekezaji ulitaka kufanywa na kampuni ya PMM katika eneo la mitaa ya Mnyamani na Kifaru, Buguruni, lakini mradi huo umesimama. 
Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipongezana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sillo mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika 
siku ya Jumapili jioni  Octoba 2, 2016 
 katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani.
Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Msongela Palela wakifurahia jambo mwishoni mwa mkutano huo 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akifunga mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kwa kuendesha vizuri mkutano huo
Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edwars Mpogolo akimpongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa mkutano kwenda vizuri
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifurahiwa na Wananchi wakati akiondoka baada ya mkutano wake wa hadhara aliofanya katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani, leo jioni. Picha zote na Bashir Nkoromo-wa theNkoromo Blog

No comments: