Advertisements

Monday, October 31, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI KENYA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS UHURU KENYATTA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Kenya.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta, alipowasili Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya, Mh. Willam Ruto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya kaburi la Muasisi na Rais wa Kwanza wa Kenya Maremu Mzee Jomo Kenyatta mara baada ya kuweka shada la maua katika eneo la katikati ya jiji la Nairobi nchini Kenya mara baada ya kuwasili nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wa dua katika eneo la kaburi hilo la Muasisi na Rais wa Kwanza wa Kenya Maremu Mzee Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa nyimbo za mataifa mawili zikiwa zinapigwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima aliloandaliwa na Jeshi la Kenya mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na ujumbe wake katika Ikulu ya Nairobi.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mbalimbali wa Kenya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata nchini Kenya. PICHA NA IKULU.

1 comment:

Mamy said...

Hongera Mh.Rais kwa kwenda kwa watani zetu wa jadi.binafsi nimependezwa na protocal ya picha kwa maana ya kuwapa nafasi viongozi bila muonekano wa wapambe wengine nyuma yao kwa kweli inapendeza sana. Kuna jambo la kujifunza kwenye itifaki ya upigaji picha. MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU NA WATU WAKE