ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 4, 2016

SHIRIKA LA MAGEREZA NA MFUKO WA PPF WAINGIA UBIA WA UJENZI WA KIWANDA KIPYA CHA VIATU HAPA NCHINI

Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) akizungumza katika hafla fupi ya utiwaji saini wa Mkataba wa wa Uwekezaji wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza Karanga, Moshi baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa Jamii wa PPF(kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio, Oktoba 4, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio(kushoto) na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) kwa pamoja wakisaini Mkataba wa Uwekezaji baina ya Taasisi hizo mbili katika Ukumbi wa Mkao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar salaam, Oktoba 4, 2016
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio wakibadilishana nyaraka mbalimbali za Makubaliano katika Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya utiwaji saini wa Mkataba wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha Viatu.
Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Mfuko wa Jamii wa PPF wakifuatilia utiwaji saini wa Mkataba wa Uwekezaji.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiwaji wa Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

1 comment:

African Queen said...

Hongera PPF kwa kuja na mradi very strategic.
Kwanza viatu ni hitaji la kila Mtanzania wa leo,
wakubwa kwa wadogo,wazee kwa vijana,raia,
wanajeshi, wafungwa n.k.Kwani viatu sio pambo,
iio hereni, sio saa ni AFYA na ni KITENEA kazi!
Pili ubia mlioingia nao ni wa aina yake na kupongezwa -
Public Public Partnership.
Tanzania itajengwa na wenye moyo.