Advertisements

Tuesday, November 8, 2016

KUTOKA NEW YORK CITY NYUMBANI KWA WAGOMBEA URAIS WA MAREKANI HILLARY CLINTON NA TRUMP


 Shomari kutoka V.O.A Swahili ya Washington. DC akiwa na Ny Ebra wa vijimamboblog mbele ya jengo la Javits Center New York City. Javits Center hipo 34 Street na 11 ave ndiyo kituo cha Hillary Clinton atakachopokelea mtokeo ya kura  za urais. Javits Center ni block 19 kutoka Hilton Manhattan hotel, 6 Ave ambako Trump nae atakuwepo kusubiri matokeo yake pia. Ni mshike mshike wa ulinzi New York kwakweli kwani haijawai kutokea wagombea wa urais Marekani kutokea jiji moja. Nakusubiri matokeo ndani ya borough moja Manhattan, New York ina borough 5 ambazo ni Manhattan, Bronx, Brooklyn, na Staten Island.
Shomari  wa V.O.A akiwa ndani ya Javits Center kwenye kambi ya Hillary Clinton kuwa letea matokeo hayo live bila chenga.

Timu mzima ya V.O.A ndani ya nyumba.


 Katika ni Mtangazaji wa kituo cha radio kutoka Peru akiwa New York nae kuwajuza wale walio Peru chochote kitakacho tokea kwenye matokeo ya urais kati ya Hillary Clinton na Trump.

Hapa ni shabiki wa mama Clinton akiwa na bendera yake.
Times Square kituo cha TV cha ABC kitarusha matokeo hayo live 


No comments: