Kushoto ni meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi Asa Mwaipopo akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama Novemba 1,2016 wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama lengo ni kusaidia hospitali hiyo kuboresha huduma zake za fya kwa jamii.
Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Nyuma ni mkuu wa kitengo cha Afya na Usalama Kazini katika mgodi wa Acacia Buzwagi, Dkt. Antoinette George. Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Kahama Dkt. Bruno Minja akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ambapo alisema hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama inahudumia wagonjwa kutoka halmashauri zote za wilaya ya Kahama ambazo ni mji Kahama ,Ushetu na Msalala pia wagonjwa kutoka maeneo ya wilaya ya Shinyanga,mkoa wa Tabora (Urambo,Kaliua,Nzega) na Geita. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama,Anderson Msumba akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliupongeza mgodi wa Acacia Buzwagi kwa msaada huo na kuongeza kuwa Buzwagi wamekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Kahama kutokana na kujitokeza mara kwa mara kusaidia jamii katika masuala mbalimbali. Meneja mkuu wa mgodi wa Acacia Buzwagi Asa Mwaipopo alisema kampuni ya Acacia imetoa msaada wa vifaa tiba hivyo kufuatia ziara ya kawaida aliyoifanya akiwa ameambatana na Mkuu wa kitengo cha Afya na Usalama kazini katika mgodi wa Acacia Buzwagi,Dkt. Antoinette George katika hospitali hiyo na kujionea mapungufu ya vifaa tiba katika hospitali hiyo. Mwaipopo alivitaja vifaa tiba hivyo kuwa ni mashine tatu maalumu za oksijeni,viti vitano vya magurudumu kwa ajili ya wagonjwa,machela mbili za kisasa zenye magurudumu,mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa na mashine mbili maalum za umeme za kusafishia vifaa vya upasuaji(Autoclave Mashines).Wa kwanza kushoto ni Katibu tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya. Watoa huduma katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama.Kulia ni mganga mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama, Dkt. Joseph Ngowi. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimsikiliza meneja mkuu wa mgodi wa Acacia Buzwagi Asa Mwaipopo. Wafanyakazi katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama wakifuatilia zoezi la kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na mgodi wa Acacia Buzwagi Kulia ni meneja wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi, Asa Mwaipopo akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa. Mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa iliyotolewa na mgodi wa Buzwagi katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama. Kulia ni meneja wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi, Asa Mwaipopo akikabidhi moja ya mashine maalumu ya kutengenezea oksijeni kati ya mashine tatu zilizotolewa na mgodi huo. Mashine ya kutengenezea Oksijeni iliyotolewa na mgodi wa Acacia Buzwagi. Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Acacia Buzwagi, George Mkanza akiwa amekaa katika kiti cha wagonjwa wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba huku furaha ikitawala eneo hilo .Mgodi huo umetoa viti vitano vya magurudumu kwa ajili ya wagonjwa. Kiti cha magurudumu kwa ajili ya wagonjwa. Meneja wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi Asa Mwaipopo akikabidhi mashine maalumu ya umeme ya kusafishia vifaa vya upasuaji (Autoclave mashine).Acacia Buzwagi wametoa mashine mbili maalumu za umeme kwa ajili ya kusafishia vifaa vya upasuaji. Mashine maalumu ya umeme ya kusafishia vifaa vya upasuajiKushoto ni Mashine ya Oksijeni,kulia ni machela za kisasa zenye magurudumu. Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza baada ya kupokea vifaa tiba vilivyotolewa na mgodi wa Acacia Buzwagi ambapo aliushukuru mgodi wa Buzwagi kwa kuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii na kuwaomba kutochoka kuwasaidia wananchi. Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyakazi katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama kutunza vifaa hivyo na kuvitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa na siyo vinginevyo.Kulia ni waandishi wa habari wakichukua matukio Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu alitoa wito kwa wadau wa maendeleo kujitokeza kusaidia hospitali na vituo vya afya kwani bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali. Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliuomba mgodi wa Buzwagi kuendelea kushirikiana na halmashauri hiyo kusaidia jamii.
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia mgodi wake wa Buzwagi imekabidhi vifaa tiba vya kisasa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 22,410,000/= kwa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama kwa ajili ya kuisaidia katika kuboresha huduma zake za fya kwa jamii. Vifaa vilivyokabidhiwa ni mashine tatu maalumu za oksijeni,viti vitano vya magurudumu kwa ajili ya wagonjwa,machela mbili za kisasa zenye magurudumu,mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa na mashine mbili maalum za umeme za kusafishia vifaa vya upasuaji. Akikabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa hospitali hiyo, meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo alisema wametoa msaada huo baada ya uongozi wa Acacia kutembelea hospitali hiyo na kujionea mapungufu ya vifaa tiba. “Kutokana na kwamba kuwajibika kwa watu wetu na jamii inayozunguka imekuwa utamaduni wetu,tulifanya kikao na baadhi ya viongozi wa hospitali hii,walionesha nia ya kuhitaji msaada ili kukabiliana na changamoto za tiba”,alieleza Mwaipopo. “Kama sehemu ya mpango wa sera yetu ya mahusiano ya jamii,leo tunakabidhi vifaa hivi ambavyo tunaamini vitasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za tiba kwa wagonjwa na kuleta ahueni kwa wagonjwa na pia vitawasaidia madaktari waweze kutoa huduma kwa wagonjwa wengi zaidi ili kuokoa maisha ya watu wengi zaidi”,aliongeza Mwaipopo. Akipokea msaada huo,mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu mbali na kuupongeza mgodi wa Buzwagi kwa msaada huo,pia aliwataka viongozi wa hospitali hiyo kutunza vifaa hivyo vya kisasa na kutumia kwa matumizi yanayotakiwa kwani wananchi wengi wanahitaji huduma. Naye mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Kahama Dkt. Bruno Minja aliushukuru uongozi wa Buzwagi kwa msaada huo ambao umelenga moja kwa moja kuboresha huduma kwa wagonjwa na kurahisisha utoaji huduma kwa watoa huduma. Minja alisema watavitumia vyema vifaa hivyo hususani katika huduma ya mama na mtoto,huduma za upasuaji na huduma za dharura ikiwemo ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikijitokeza.
Mwishoni mwa mwaka 2015 mgodi wa Buzwagi pia ulikabidhi vifaa tiba mbalimbali katika kituo cha afya cha Mwendakulima kilichojengwa na mgodi huo ambapo ujenzi wa kituo hicho chenye kitengo cha afya ya mzazi na mtoto (RCH) na kitengo cha kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD) pia ulihusisha ujenzi wa nyumba za wafanya kazi.
Mgodi wa Buzwagi umeweka huduma ya umeme wa solar katika kituo hicho na nyumba za wafanyakazi,huduma ya kukinga maji ya mvua na kuyahifadhi.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment