Advertisements

Tuesday, November 1, 2016

Shirika la ndege lamwaga ajira 425,00 barani Afrika

Abu Dhabi. Idara ya anga ya Shirika la Etihad kwa kushirikiana na wadau wake, wanatarajia kutoa takriban fursa 425,000 za ajira ikiwa ni pamoja na kutoa Dola za Marekani 3.6 milioni.

Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Uchumi ya Oxford, inabainisha kwamba Idara hiyo ya Anga pamoja na wadau wake wana mchango wa kukuza uchumi barani Afrika na duniani.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba, Idara hiyo ya anga (EAG) na wadau wake wanatarajia kuchangia Dola za Marekani 1.1 bilioni katika uchumi na Sekta ya Utalii Dola 2.5 bilioni.

Licha ya hayo, zitatolewa ajira 117,000 na zingine 308,000 kupitia sekta ya utalii.Mwaka huu, Shirika la Etihad limejiwekea malengo kutoa huduma bora kwa wateja na kuongeza ufanisi katika vituo vya kusafirisha mizigo duniani kote.

Wanatarajia kuhudumia abiria milioni 19 kwa kutumia ndege 100,000 ambazo kati ya hizo, ndege 83,000 zitafanya safari za Amerika kwa abiria 1.1 milioni kutoka duniani kote.

Tangu kuzinduliwa kwa safari yake ya kwanza kwenda Misri mwaka 2004, Etihad ilipanua wigo wa huduma zake barani Afrika, sambamba na ufunguzi wa vituo vingine zaidi katika nchi nane zingine zikiwamo Afrika Kusini, Morocco, Libya, Sudan, Kenya, Nigeria, Uganda na Tanzania.

Kiasi cha Dola 1.1 bilioni kilichotolewa, kinatokana na shughuli zinazofanywa na idara hiyo ya anga duniani kote, pamoja na mchango wa wadau wake.

Katika mchango huo, Idara ya Anga pekee inatarajiwa kuchangia Dola 400 milioni na fursa za ajira 39,000 mwaka huu. Kiasi hicho cha fedha kwa sehemu kubwa kitategemea bidhaa zitakazouzwa barani Afrika.

Ofisa mtendaji mkuu wa idara ya anga ya Etihad, James Hogan alisema, “Fursa za ajira zilizotolewa katika utalii, sekta ya usafirishaji na huduma za vyakula, zinatokana na uwepo wa Idara ya Anga katika soko letu la Afrika. Pia ni ishara ya kukua kwa sekta ya usafirishaji.”
MWANANCHI

No comments: