Advertisements

Tuesday, November 1, 2016

Tanzania kuanza kuvuna maji ya mvua

By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Maji na Umwagiliaji Gerson Lwenge amesema Serikali imeanza mpango wa kujenga mabwawa maalumu kwa ajili ya kuvunia maji ya mvua ili kukabiliana na uhaba wa maji unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Lwenge ameyasema hayo leo (Jumanne), wakati akizindua mkutano wa Muungano wa Wadhibiti wa Huduma za Maji Kusini na Mashariki ya Afrika (Esawas).

Amesema maji hayo yakivunwa yatatumika katika kilimo cha umwagiliaji na kunywesha mifugo na matumizi mengine makubwa.

"Tanzania tumechelewa sana kuanzisha mpango huu ndiyo maana tunataka kwenda haraka ili tuanze kunufaika na maji ya mvua," amesema.No comments: