Advertisements

Monday, November 14, 2016

THABO MBEKI ATETA NA MAGUFULI IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki Ikulu.

By Mwandishi wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Pombe Magufuli Novemba, 2016 amekutana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki leo Ikulu na kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu Umoja wa Afrika (AU).

Pamoja na kuzungumzia masuala yahusuyo Umoja wa Afrika, Rais Mbeki amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Mstaafu Thabo Mbeki pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozifanya katika uongozi wa nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja aliokuwa madarakani.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu Mbeki kwa kumtembelea na kufanya nae mazungumzo na pia amempongeza kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Usomi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
No comments: