Advertisements

Monday, November 14, 2016

WADAIWA SUGU BODI YA MIKOPO WAPEWA SIKU 30

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wadaiwa sugu 142,470 wenye mikopo ya shilingi 239,353,750,170.27 iliyokwishaiva hawajajitokeza wala kuanza kulipa mikopo yao.

Akitolea ufafanuzi wa maana ya neo "Wadaiwa Sugu", Badru amesema kuwa ni wanufaika waliokopeshwa, muda wa matarajio ukapita bila kuwasilisha taarifa zao na kulipa madeni ya mikopo waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/1995.

Kuhusu hatua zinazochukuliwa na bodi hiyo, Badru amesema mbali na kutoa siku 30, bodi hiyo inakamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa kuvunja sheria ya bodi ya mikopo kifungu cha 19A(1).

Hatua nyingine ni pamoja na kuyawasilisha majina hayo katika taasisi za mikopo, kuwasiliana na wadhamini wao pamoja na kuyatangaza hadharani majina ya wadaiwa sugu wote ili waajiri, wadhamini na wadau wengine wayajue na kutoa taarifa katika bodi hiyo.


Kuhusu takwimu za mikopo iliyotolewa, amesema tangu 1994/95 hadi 2015/16 jumla ya shilingi 2,595,932,575.56 zimekopeshwa kwa jumla ya wanufaika 379,179.

Amesema kati ya mikopo yote iliyokopeshwa, mikopo iliyoiva ni shilingi 1,425,708,285,046.48 kwa wanufaika 238,430 ambao tayari wamemaliza kipindi chao cha matazamio.

Badru amesema kuwa jumla ya wanufaika wa mikopo 93,500 wamebainika na kupelekewa ankara za madeni yao, ambapo kati yao wanufaika 81,055 wanaendelea kulipa.

1 comment:

Anonymous said...

Hawa bodi ya mikopo wanatania. Waalikuwa wapi miaka yote kufuatilia haya madeni? Tulisign mikataba na wafadhili wetu wakasign pia hembu watuonyeshe hata barua moja waliokwishawahi kuituma kwa hawa watu wanaotuita wadaiwa sugu na hawakulipwa? Walituma mwakilishi Marekani wakati wa kongamano la DICOTA na akapewa nafasi ya kuongea na akakumbusha suala hili la wanadiaspora hapa Marekani wanaodaiwa wakajitokeza na kujaza fomu iliyokuwa inataka habari zako kamili, email number ya simu ili atakaporudi Tanzania aangalie madeni yetu na kutuma. Hadi leo mimi sijapata mawasiliano yeyote yale. I think the issue is not kutolipa but the issue is there was no system put in place for us to pay back... Hata haya matangazo still hayasemi how and where to pay. Publish hayo majina na madeni then Wekeni bank information, M-pesa na mikopo italipwa. No need ya kuweka heading calling people wadaiwa sugu!