Advertisements

Wednesday, January 11, 2017

IMF yadai uchumi wa Tanzania ni poa, lakini yaonya ubanaji wa matumizi

Bodi ya Utendaji ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeeleza kuwa hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri.

Bodi hiyo imeeleza hayo baada ya kumaliza kufanya tathmini ya hali ya uchumi hapa nchini, chini ya Mradi wa miaka mitatu wa Kuwezesha Sera (PSI). Katika taarifa yao iliyochapishwa katika tovuti, bodi ilisema kuwa ukuaji wa uchumi, ulikuwa vizuri katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 na hivyo kuleta matumaini ya kubaki katika ukuaji wa asilimia saba kwa mwaka huu wa fedha.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa bei za bidhaa zilishuka kufikia chini ya malengo ya asilimia tano. Hata hivyo, imetahadharisha kuwa kuna madhara ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wa uchumi, ikiwemo msimamo mkali wa sasa juu ya sera zinazohusu uchumi mdogo.
Aidha, bodi imependekeza kuwa hali uchumi mdogo kwa sasa inapaswa kutafutiwa ufumbuzi, ikiwemo kulegeza msimamo katika sera za muda mfupi. Hata hivyo, taarifa ya bodi hiyo inasema baada ya kupata ongezeko dogo kufikia Julai hadi Septemba, serikali ijizatiti kuongeza juhudi katika kutekeleza bajeti, na hasa katika uwekezaji wa kijamii.
Sehemu ya ripoti hiyo inasema:
There are risks that could adversely affect economic growth going forward, arising from the currently tight stance of macroeconomic policies, the slow pace of credit growth that may become protracted, slow implementation of public investment, and private sector uncertainty about the government’s new economic strategies. Monetary policy should be eased to address the tight liquidity situation and support credit to the private sector
Aidha imeeleza kuwa juhudi zilizofanywa na serikali katika kupambana na rushwa na ukwepaji wa kulipa kodi, zimesaidia kuweka msingi mzuri kwa kuongeza uwekezaji katika miundombinu kuanzia bajeti ya mwaka 2016/17.


Chanzo:Habari Leo

No comments: