Advertisements

Tuesday, January 10, 2017

Mimi ni mgombea katika shindano la Mr & Ms ASA, Maryland, litakalofanyika Jumamosi Januari 28, 2017 naomba kura yako

Kama wengi mnavyojua mimi ni mgombea katika shindano la Mr & Ms ASA, Maryland, litakalofanyika Jumamosi Januari 28, 2017 katika chuo kikuu cha Bowie State. Huku siku ya shindano lenyewe ikiwa inakaribia nina maelezo mapya.


Upigaji kura kwa njia ya mtandao unaanza Jumatatu, Januari 9 katika tovuti ya marylandasa.com

Tafadhali hakikisha unaniunga mkono pamoja na #TeamJumbe

Natumia shindano hili kama jukwaa la kutangaza nchi yangu ya asili Tanzania 🇹🇿 na kufundisha watu sehemu ya utamaduni, mila na muziki wetu. Najulikana kama Mr. Tanzania kwa hiyo ni wajibu wangu kuwakilisha, nchi yangu, mizizi yangu. Siwezi kufanikisha hili bila msaada wako. Naweka moyo wangu katika muziki na kila ninachofanya si kwa ajili yangu tu au wazazi wangu, au familia yangu bali ni kwa watu wangu & na nyinyi ndio watu wangu mnaonipa motisha. Bila nyinyi na uungaji mkono wenu siwezi kwenda mbele. Sisi ni wamoja kwa hiyo lazima tuungane mkono na kuwa pamoja katika hali na mali. Shindano hili ni fursa kuonyesha watu kutoka mataifa mbali mbali ya Afrika na kwingineko Tanzania ni nini, tunahitaji kuonyesha uwepo wetu juu ya jukwaa na katika safu za ushangiliaji. Natumaini utaniunga mkono.

Tafadhali kumbuka upigaji kura mtandaoni unaanza Jumatatu, Januari 9 katika marylandasa.com.

Baada ya Januari 14 tiketi zinaweza kupatikana mtandaoni kwa $15.

Muunge mkono Mr Tz #TeamJumbe 🇹🇿....Asili Haipotei

No comments: