ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 12, 2017

UZINDUZI WA KAMPENI YA KUINUA MAADILI KITAIFA

Mwanaharakati Mayrose Kavura Majinge kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameandaa Kampeni Maalum ya Kuinua Maadili Kitaifa itakayofanyika kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 2017.
Lengo la kampeni hii ni kuinua na kudumisha maadili ya waTanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha mfumo wa muundo wa jamii yetu ya Kitanzania.
Kampeni hiyo itaendeshwa kwa njia ya midahalo, usaili, tafakari kwa kutilia mkazo maelezo ya kitabu kiitwacho: “Chombo Muhimu kwa Maendeleo Yako” 
Uzinduzi huo utafanyika:
Tarehe: 14 Januari, 2017 
Muda: Saa 9:00 Alasiri – 10:00jioni (3:00 - 4:00 pm ET)
Mahali: 6733 New Hempshire Avenue, 
             Takoma Park, MD 20912
Lengo la Kampeni: Kuinua maadili mema kwa ajili ya kujenga mfumo bora katika kuendesha maisha yetu ya kila siku.
Kauli Mbiu ya Kampeni: “Maadili mema na mfumo bora katika jamii vinaanza na mimi na wewe, tujielekeze kwenye ukweli huu tujenge maisha yenye tija”
Kwa habari zaidi piga namba: 703 981 1323
Tanzania itajengwa na watanzania.
Karibuni sana.

No comments: