ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 1, 2017

IZARA YA MALIASILI NA UTALII YAWAPIGA MSASA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA ARDHI,MALIASILI NA UTALII KUHUSU CHANGAMOTO ZA UHIFADHI WA WANYAMAPORI NCHINI

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Kanyatta akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi kunavyoathiri sekta ya utalii katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Yussuf Hussein, akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu utalii wa baharini ambao umekuwa haupewi kipaumbele katika kutangazwa pamoja na kuendelezwa katika semina hiyo
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Marwa Chacha, (katikati) akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu wanyamapori waharibifu wa mazao kama vile tembo wanavyoathiri maisha ya wapiga kura wake kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye, (katikati) Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ( kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ( wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa makini michango ya wajumbe wa kamati hiyo wakati walipokuwa wkichangia hoja kuhusu mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini, iliyofanyika jana mjini Dodoma
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Devota Minja, MB ( wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa Wizara hiyo kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Kwa upande wa kushoto ni viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) pamoja na na viongozi wa taasisi katika semina ya kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii iliyofanyika jana mjini Dodoma

1 comment:

Anonymous said...

Dukuzi za Faru John zimeishia wapi? Au ndio kama kawaida mtindo wa kuibua na kusahau. Kama.ilivyokuwa Mgawo wa mil. 10 kila mbunge wa Chama chetu na hadi leo takukuru waliahidi kuleta Majumuisho bado kitendawili. Daah hii ndio TZ yetu!!