ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 15, 2017

MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA WAWAOMBA WANANCHI WASAIDIE WATU WASIOJIWEZA

NA MWANDISHI MAALUM

MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa wito kwa Watanzania kujengea utamaduni wa kutembelea vituo vya wazee na watu wenye mahitaji maalumu na kutoa misaada ili waweze kujikimu.

Wameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Amani Ipuli yaliyoko kwenye Manispaa ya Tabora mkoni Tabora.

Katika makazi hayo wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage pamoja na mafuta maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule mbalimbali mkoni Tabora.

Hata hivyo, Mama Janeth amewapongeza watumishi wote wanaofanyakazi kwenye makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu kwa sababu kazi hiyo ni ngumu na ina changamoto nyingi.

“Ibada si kwenda katika nyumba za ibada pekee bali hata kuwatembelea wazee, watu wenye mahitaji maalumu na wasiojiweza utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu. Nawaomba tujitahidi kuwatembelea,” amesema.

Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wananchi wote wawe na utaratibu wa kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulele wazee, walemavu na wasiojiweza nchini na kuwafariji kwa sababu wanahitaji upendo na faraja kutoka kwao.

Pia Mama Mary ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa hali mali katika kuwahudumia wazee na watu wenye mahitaji maalumu.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amesema Serikali itahakikisha huduma zinaboreshwa katika makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu nchini kwa kuwa vingi viko katika hali mbaya.

Awali Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Tabora, Bw. Baraka Makona alisema makazi hayo yalianzishwa mwaka 1969 kwa lengo la kuwasaidia watu wasiojiweza hususan walioathirika na ugonjwa wa ukoma ambao walitengwa na familia zao.

Bw. Makona alisema baada ya ugonjwa wa ukoma kupungua mkoani Tabora kwa sasa makao hayo yanahudumia wazee wasiojiweza wenye ulemavu na ambao wametengwa na jamii kutokana na sababu mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Bw. Makona alisema makazi hayo yanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa majengo, ukosefu wa gari la wagonjwa hali inayosababisha usumbufu mkubwa hasa inapotokea dharura nyakazi za usiku kwani hakuna zahanati karibu na makazi hayo.

Pia Bw. Makona amewapongeza wake wa viongozi hao kwa moyo wao wa dhati wa kuamua kutembelea makazi hayo na kutoa misaada mbalimbali vikiwemo vyakula kwa sababu wameonyesha matendo ya huruma na Mwenyezi Mungu atawabariki.

Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee George Busambilo aliwashikuru wake hao wa viongozi kwa niaba ya wenzake na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Queen Mlozi wakati yeye na Mama Mary Majaliwa walipotembelea katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa nderemo walipowasili katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi pamoja na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa Pamoja na naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hamisi Kigwangwalla wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa tabora Mhe. Aggrey Mwanri akianzisha harambe kwa ajili ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwakabidhi mafuta maalumu wawakilishi wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi walioalikwa kwenye hafla iliyofanyika katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017

No comments: