ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 23, 2017

KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA MUFINDI JIMSON MHAGAMA AJITOSA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI.

Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama  akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni wa kumtafuta diwani wa kata ya Igombavanu wilayani mufindi akikitumikia chama.
 Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama  akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni akimwombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli mwaka 2015 katika uwanjwa wa wambi mafinga.
 Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama  akipeana mkono na waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne mh Mizengo Pinda kwenye moja ya majukumu ya kukitumikia chama.
Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama  akipeana mkono na Rais mstaafu wa awamu ya nne dr Jakaya Mrisho Kikwete na kubadilishana maneno ya hapa na pale

 Na Fredy Mgunda, Mufindi

KATIBU wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama ametangaza nia ya kugombea nafsi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa bunge la afrika mashariki kwa kuiwakirisha Tanzania.

Akizungumza kwa njia ya simu Mhagama alisema kuwa atahakisha lugha ya kiswahili inatumika barani afrika kama lugha mama kwa kuwa ndio lugha ilisamba zaidi barani afrika.

“Nimetembea nchi nyingi hapa afrika nimekutana na watu wengi wanazungumza Kiswahili hivyo hoja yangu itakuwa kuahakikisha natimiza kitu alichotuachia hayati baba wa taifa mwalimu Julias Kabarage Nyerere”.alisema Mhagama

Mhagama alisema kuwa atalazimaka kuwatetea wakulima kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania wengi ni wakulima na uchumi wetu bado unategemea kilimo hivyo ni lazima kuwekeza nguvu kwenye kilimo chenye tija na kufanikiwa kuinua mazao yanayozalishwa hapa nchi na kukuza uchumi.

“Tanzania tumebatika kuwa na ardhi nzuri na kubwa ambayo kwa asilimia kubwa bado haijatumika kwa mjibu wa wataalam wa kilimo hivyo ni lazima kutafuta nja mbadala ya kuwainua wakulima hawa ili kuviwezesha viwanda vyetu kupata mali ghafi nyingi na za kutosha ili kuinua kipato cha kila sekta hapa nchi”.alisema Mhagama

Aidha Mhagama amewataka watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi anazozifanya kwa kutafuta njia bora ya kuinua uchumi wa wananchi wake kutoka hapaulipo hadi kufikia uchumi wa viwanda kama sera yake alivyoielekeza kwenye Tanzania ya viwanda.

“Angalia sasa tunapata wawekezaji wengi kwenye sekta ya viwanda hii ni dalili nzuri ya kuukalibia uchumi wa viwanda hivyo nikiwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki nitandelea kuunga mkono Rais kwa kutafuta njia za kuwanua wawekezaji wazawa ili waboreshe na kuanzisha viwanda vyao”.alisema Mhagama

Mhagama aliwaomba watanzania kwa ujumla kumuombea ashinde kiti hicho ili aweze kuiwakirisha vyema nchi kwa uadilifu uliotukuka

No comments: