Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa na Askari wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake, katika Ukumbi wa Bwalo la Magereza, mjini Kilwa mkoani Lindi. Masauni aliwataka maafisa na askari hao kuongeza nguvu zaidi katika ukamataji wa wahamiaji haramu pamoja na wauza dawa za kulevya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anakagua Makazi ya askari Polisi, Mitwero mkoani humo ambapo nyumba za askari hao zimechangaa na chache kutokana na wingi wa askari hao. Hata hivyo, Serikali hivi karibuni inatarajia kujenga nyumba mpya katika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni eneo la Mitwero mkoani humo ambalo nyumba za makazi ya askari polisi zitakapojengwa. Masauni alikagua nyumba wanazoishi askari hao kwasasa pamoja na kukagua eneo hilo makazi mapya yatakapojengwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akilikagua Jengo jipya la ghorofa la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi ambalo linajengwa mjini humo. Kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, George Kombe, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga. Masauni aliongozana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anaangalia ramani ya ujenzi wa makazi ya askari polisi eneo la Mitwero mkoani humo. Masauni yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi.
No comments:
Post a Comment