Naibu Waziri ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akipongeza miradi ya muungano kisiwani Pemba, wakati wa Ziara yake ya kutembelea Miradi Hiyo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya ChakeChake Bi Salama Mbarouk.
Mratibu wa Mradi wa TASAF kisiwani Pemba Bw. Mussa Said Kissenge akielezea utekelezaji wa majukumu ya Mradi huo kisiwani pemba Kwa Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake (hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Huyo ya kutembelea Mirani ya Muungano kisiwani Pemba.
Na Evelyn E. Mkokoi – Pemba
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masula ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameipongeza Miradi ya tasisi za Muungano Kisiwani Pemba, kwa kile alichodai, kutekelezeka kwa asilimia kubwa na kutatua kero za wananchi.
Naibu Waziri Mpina Aliyasema hayo Kisiwani Pemba katika ziara yake ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa chini ya taasisi za muungano na mashirika ya TASAF na MIVARF, ikiwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa soko, barabara, hospitali shule, ujenzi wa mabwa, matuta kama makingio ya maji ya chumvi yanayosaidia kuhimili madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na miradi mbali mbali ya maendeleo.
Mpina aliwataka wakazi wa kaskazini na kusini Pemba kwa Pamoja kushirikiana na waithamini na kuitunza miradi hiyo inayotekelezwa kwa thamani ya shilingi za kitanzania Bilioni 14.297,na kusema kuwa ina manufaa kwa wakazi hao, na itaweza kudumu na kuwasidia kwa muda mrefu, akitolea mfano wa barabara yenye urefu wa kilometa 80 iliyojenjwa kusini Pemba.
Alipotembelea mradi wa umeme unaopita chini ya Bahari kutoka mkoani Tanga, Mpina alisema kuwa, awali kisiwani Pemba umeme ulikuwa unawafikia watu wachache, lakini kwa sasa umeme umekuwa ni wa Bei nafuu wa uhakika naunawafikia watu wengi.
Katika Ziara yake kisiwani Pemba, Naibu Waziri Mpina Pia alitembelea jengo la Makazi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Kusema kuwa jengo hilo linatakiwa kutengewa fedha maalumu kwa ajili ya ukarabati, “viongozi wetu wakifanya kazi katika mazingira mazuri itaongeza ufanisi katika utendani wao.” Alisisitiza Mpina.
Naibu Waziri Mpina takuwepo kisiwani Unguja na Pemba kutembelea na kukagu miradi ya Muungano.
Katika Picha ni moja ya tuta lililojengwa na mradi wa TASAF kisiwani Pemba, kunusuru maji ya chumvi kuingia katika mashamba ya wakulima na kuharibu mazao kisiwani Pemba, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya Muungano.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina akichanganya Saruji na mchanga kuwasaidia mafundi wanaojenga bwawa la kuhifadhia maji ya mvua, litakalotumika kuhifadhi maji kwa matumizi ya kilimo na mifugo kisiwani Pemba, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa miradi ya Muungano chini ya TASAF.
Katikati Injinia Said Kiure, wa Kiure Contraction ya Kisiwani Pemba, akimuelezea jambo Naibu Waziri Mpina, kuhusu ujenzi wa soko la wilaya ya Mwanakwerekwe linalojengwa chini ya mradi wa Muungano wa MIVARF.kushoto ni Mkurugenzi msaidizi Idra ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Lupi Mwaikambo.
No comments:
Post a Comment