Advertisements

Monday, March 20, 2017

UMOJA WA WATANZANIA NORTH CAROLINA (UTNC) WAFANYA UCHAGUZI WAPATA VIONGOZI WAPYA

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Pendo Nyang'oro akitoa maelekezo ya jinsi ya kupiga kura kwa wanaUTNC waliofika kwa ajili ya kuwachagua viongozi wapya wa Jumuiya hiyo ya waTanzania Carolina ya Kaskazini ambao walikua wamemaliza muda wao. Uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya umefanyika siku ya Jumamosi March 18, 2017 katika hotel ya Comfort Suites jijini Durham jimbo hilo la Calorina ya kaskazini.
Viongozi wapya waliochaguliwa wakiwa katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Katibu Scholastica Kiemi, Shabani Mwapambe katibu msaidizi, Bi. Pandwe kalala mweka hazina, Saburi Mtazaraki mjumbe, Bi Gloria Alex mwenyekiti na Magayo Newa Harrison  mweka hazina msaidizi.. Mwingine ni mjumbe Samwel Temu (hayupo pichani)

No comments: