ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 12, 2017

BENKI YA AFRIKA(BOA) YAWAKUTANISHA WAANDISHI WA HABARI NA WAHARIRI KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 10 TANGU KUANZISHWA KWAKE

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Afrika (BOA), Ammishaddai Owusu-Amoah akizungumza na waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na maadhimisho ya miaka kumi ya Benki ya Afrika  (BOA) tangu kuanzishwa kwake hapa nchini Tanzania kwenye mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Picha na Geofrey Adroph

Benki ya Afrika (BOA) nchini Tanzania  imewakutanisha waandishi wa habari pamoja na wahariri kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa benki hiyo hapa nchini. Mkutano huu ulikuwa na lengo la kuweka mahusiano mazuri kati ya benki hiyo na waandishi wa habari ili kufikia malengo waliyojiwekea kwa kipindi chote cha uanzishwaji wa benki hiyo haa nchini.

Baadhi ya waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza maswali kwenye mkutano ulioandaliwa na Benki ya Afrika (BOA) kwenye maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa kwa benki hiyo hapa nchi Tanzania.
Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Afrika Tanzania (BOA), Wasia Mushi akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari pamoja na wahariri wa habari waliyokuwa wanayauliza  kwenye mkutano ulioandaliwa na benki hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka kumi ya uanzishwaji wa benki hiyo hapa nchini Tanzania.
Baadhi ya waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza kinachoendelea kwenye mkutano ulioandaliwa na benki ya Afrika(BOA) leo wakati wa maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini.
Mkutano ukiendelea 

No comments: