Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.
Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia azma ya serikali katika kujenga Tanzania ya viwanda kwa kusaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda nchini kwa kutoa mikopo nafuu kwa wakulima nchini.
Azma hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila wakati wa utiaji saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazinana Benki hiyo katika hafla iliyofanyika Ofini kwa Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.
Bibi Kurwijila amesema kwamba TADB itakeleza kwa vitendo juhudi za Serikali za Kujenga Uchumi wa Viwanda kwa kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo, mifugo, samaki na misitu ili kuongeza tija ya kilimo hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini.
“Benki imepitia upya mpango mkakati wake katika kutoa mikopo ili kuwezesha kufikia wakopaji wengi zaidi ili kuweza kufikia lengo la kuleta maendeleo katika sekta ya kilimo hasa katika kuongeza tija ya kilimo hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini,” alisema Bibi Kurwijila.
Bibi Kurwijila ameongeza kuwa katika kuchagiza malengo hayo, TADB imejpanga katika Kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya upembuzi wa miradi ya Maendeleo ya Kilimo na Umwagiliaji nchi nzima ili kubaini mahitaji halisi ya fedha na pia kusaidi kupanga maeneo ya vipaumbele ili kuanza kutoa mikopo hasa kwa utaratibu mahsusi.
Ametaja malengo mengine ya kimkakati ya TADB ni pamoja na kuboresha huduma kwa kuanzisha mazao maalum ya huduma za kibenki kwa wakulima wadogowadogo kulingana na mnyororo husika wa thamani na pia kuanza huduma za Zaidi kupitia taasisi za fedha zilizopo (wholesale lending and Refinancing) ili kufikia wakulima wengi zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa mpaka sasa Benki imefanikiwa kukopesha jumla ya shilling bilioni 6.5 kwa vikundi 20 vyenye jumla ya wakulima 2575.
Bw. Assenga ameongeza kuwa Benki imeweza kuvijengea uwezo vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla wa wanachama 44,400 katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga.
“Kupitia mafunzo hayo TADB imewezesha jumla ya vikundi 19 kutimiza masharti na maandalizi ya msingi ya kuweza kukopa; Vikundi vingine vilivyobaki vinaendelea kupatiwa mafunzo ili viweze kufikia hali ya kuweza kukopesheka,” ameongeza.
Kwa mujibu wa Bw. Assenga, TADB imeweza kuinua idadi ya wakulima watumiao mabenki na vyombo vya fedha wapatao 2,359 ambao kati yao wanawake ni 863 sawa na asilimia 36.6 ya wanufaika.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano alisema taasisi za umma zina wajibu wa kuisaidia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ili kuleta maendeleo endelevu nchini.
Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akimuangalia Mkuu wa Huduma za Kisheria wa TADB, Bibi Neema Christina John (Katikati) wakati akiendelea na zoezi la ugongaji wa mihuri Mikataba ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano (Kushoto) akibadilishana Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (Katikati) akizungumza na Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kulia). Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto).
No comments:
Post a Comment