Mashuhuda wakiandaa mchakato wa kuchanganya kuponi katika droo ndogo iliyochezeshwa leo Jumatano kwenye Viwanja vya Bakhresa jijini Dar. Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Majjid (katikati) akiweka kumbukumbu ya majina ya washindi. Kulia ni Mhariri wa gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli na kushoto anayeshudia ni Afisa Tawala wa Global Publishers, Soud Kivea.
Mc Chaku Shemungia (mwenye kofia) akineshwa kuponi iliyoshinda na mmoja wa wananchi aliyeshiriki kuchagua kuponi ya ushindi Mashuhuda wakichanganya kuponi kabla ya kuchagua moja yenye bahati. Kuponi zikichanganywa haswa, haikuwa mchezo. Mchakato wa kuchanganya ukiendelea Mkazi wa Manzese Dar, Mgaza Mwemanga ambaye alijishindia simu ya kisasa aina ya Phantom 6 naye alipewa nafasi ya kumchagua mshindi wa pikipiki. Mwakilishi wa Kampuni ya Tecno ( Experience More), Erick Mkomoye akielezea umahiri za simu mpya aina ya Phantom 6 inayotengenezwa na kampuni yao. Mwalimu wa British School, Sekunda Pius (kulia) akimzawadia kalenda mmoja wa wasomaji aliyejishindia zawadi za papo hapo Afisa mauzo wa TING HD James Rugaimukamu akinadi king'amuzi cha kampuni hiyo. Wanenguaji wakitotoa burudani walipofika Kimara Suka muda mfupi kabla ya kuelekea Viwanja vya Barekhsa ambapo droo hiyo ilichezeshwa. Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli akiwataka wananchi kuendelea kushiriki Bahati Nasibu ya Jishindie Nyumba. Mmoja wa wasomaji akisoma jina la mshindi wa zawadi ya fulana wakati msafara wa Bahati Nasibu hiyo ulipofika Kimara Korogwe kabla ya kuelekea Manzese. Mmoja wa wanenguaji akiwachagiza wakazi wa Kimara Temboni. Mr Shinda Nyumba (kulia) akimkabidhi fulana mmoja wa wasomaji wa maeneo ya Kimara Korogwe. [/caption]
Mkazi wa Tanga Bi. Agness Lymo (54) ameibuka mshindi wa pikipiki katika droo ndogo iliyochezeshwa leo Jumatano kwenye Viwanja vya Bakhresa jijini Dar.
Katika droo hiyo kuelekea droo kubwa ya mchezo wa kubahatisha kujishindia nyumba, washindi wanne walipatikana ambapo mshereheshaji wa hafla hiyo, Chaku Shemungia alianza kuwataja washindi hao ambapo kuponi zao ziliibuka kidedea katika droo hiyo.
Katika droo hiyo alianza kutafutwa mshindi wanne ambapo baada ya kuponi hizo kuchanganywa mbele ya umati uliofurika uwanjani hapo, kuponi ya Eveline Thomas wa Keko jijini Dar ilishinda na hivyo kutangazwa kuwa mshindi wa seti ya vyombo (Dinner set).
Mshindi wa tatu alikuwa Shaban Muhindila (66) wa Morogoro aliyeibuka na tivii bapa (Flat screen).
Mashuhuda waliokuwa uwanjani hapo viroho vikiwadunga kumtaka kumjua mshindi wa pili kuponi ya Mgaza Mwemanga (56) mkazi wa Manzese jijini Dar ndiyo iliyoibuliwa ambapo ziliibuka shangwe na nderemo uwanjani hapo ambapo mshindi huyo na ndugu na jamaa zake walikuwepo kwenye viwanjani hapo.
Mgaza alijishindia simu ya kisasa aina ya Phantom 6.
Kutokana na furaha aliyokuwa nayo Mgaza ilibidi mshereheshaji Mc Chaku ampe kazi ya kuchanganya kuponi na kuichagua kuponi ya mshindi wa kwanza.
Mgaza ambaye alijinadi kuwa yeye ni msomaji mkubwa wa magazeti ya championi na Risasi aliufanya mchakato huyo ambapo bahati ya mshindi wa kwanza ilikwenda kwa Bi. Agnes Lymo (54) mkazi wa Tanga na kuhitimisha zoezi hilo.
Katika tukio hilo sambamba na Global ilishirikiana kiukaribu kukamilisha mchakato ikiwa na British School, Kampuni ya Ving'amuzi vya Ting, Tecno Exprience More na wengineo.
Sambamba na washindi hao wengine walijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo fulana, kalenda za British School nk.
(PICHA/ HABARI: RICHARD BUKOS/GPL)
No comments:
Post a Comment