Advertisements

Thursday, April 27, 2017

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. Sarah Cooke alipomtembelea leo katika ofisi za Wizara. Katika mzungumzo yao Mhe. Kolimba alieleza nia ya Serikali ya Tanzania katika kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Uingereza sambamba na kuzungumzia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali yake katika kuwaletea maendeleo na kuboresha maisha ya watanzania. 
Mhe. Sarah akimweleza Mhe. Kolimba malengo ya Serikali ya Uingereza katika kuimarisha maeneo ya ushirikiano hususan katika sekta ya kilimo, elimu, afya sambamba na ujenzi wa miundombinu. 
Mazungumzo yakiendelea, kulia ni maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Picha ya pamoja.

No comments: