Advertisements

Tuesday, April 25, 2017

Mbatia aomba wiki kumpa Mrema sukari

MBUNGE wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) amekiri kumuahidi Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party, sukari wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana na ameahidi kutekeleza ahadi hiyo.

Akizungumza kwa simu Jumamosi iliyopita, Mbatia alikiri kumwahidi Mrema sukari, lakini akaomba apewe muda wa wiki moja kutimiza ahadi yake. Akizungumzia afya yake iliyosababisha asionekane jimboni na bungeni, alisema kwa sasa afya yake imeimarika na hivi karibuni ataanza kuonekana jimboni kwake akitekeleza majukumu yake. Hatua ya Mbatia inatokana na hivi karibuni Mrema kumshitaki kwa wananchi kuwa ameshindwa kutekeleza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni mwaka juzi.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCRMageuzi kitaifa, alichukua nafasi ya Ubunge wa Vunjo baada ya kumshinda Mrema katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kwa mujibu wa Mrema, Mbatia alisema katika kipindi hicho kuwa atafanya kila linalowezekana kuhakikisha miundombinu ya jimbo hilo inakuwa sawa, lakini hilo hajatekeleza ahadi hiyo.

Kadhalika, Mrema alisema Mbatia amekuwa haonekani bungeni kwa kipindi kirefu kupeleka kilio cha wananchi. Aliwataka wananchi wa Jimbo la Vunjo kutathmini kauli aliyoitoa Mbatia kuwa yeye Mrema ni mgonjwa ili wasichague kuwa mbunge. Mrema alihoji ugonjwa unaomsumbua Mbatia na kumfanya asishiriki shughuli za maendeleo jimboni kwake wakati yeye Mrema anashughulikia kazi alizopewa na Rais John Magufuli bila ya wasiwasi. Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti Bodi ya Parole aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.

HABARI LEO

No comments: