Advertisements

Tuesday, April 25, 2017

Watu 24 wafariki ajalini Mtito Andei, Kenya BBC

Ajali
Watu 24 wamefariki na wengine kadha kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa manane katika barabara kuu ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa.

Ajali hiyo iliyohusisha basi la kubeba abiria na lori la kusafirisha mafuta ghafi ya kupikia ilitokea katika eneo la Kambu, karibu na Mtito Andei.

Mkuu wa polisi wa eneo la Kibwezi Leonard Kimaiyo ameambia BBC kuwa watu 23 walifariki papo hapo na mwingine mmoja akafariki akitibiwa hospitalini.

Watu 20 walipata majeraha na kupelekwa katika hospitali za miji ya Kibwezi na Makindu.

Bw Kimaiyo amesema walionusurika waliambia maafisa wa polisi dereva wa basi alikuwa akijaribu kupita gari jingine basi lilipogongana na lori hilo.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Uchukuzi Kenya, watu 3,000 hufariki kila mwaka kutokana an ajali za barabarani.

No comments: