Advertisements

Tuesday, April 25, 2017

NMB yakabidhi jengo la kupumzikia Wagonjwa JKCI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao wanaokwenda kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Vick Bishubo (wa kwanza kulia) wakifuatilia tukio hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kuzinduwa jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao wanaokwenda kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi akifuatilia mazungumzo hayo.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Vick Bishubo (kulia) akizungumza kabla ya uzinduzi wa jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao wanaokwenda kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kulia) pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Vick Bishubo (wa kwanza kushoto) wakielekea katika eneo la uzinduzi wa jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa JKCI.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB jana ilikabidhi Jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao wanaowaleta wagonjwa kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi jengo hilo lenye uwezo wa kuhifadhi watu 100 kwa pamoja wakiwa wamekaa kusubiri huduma, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema ujenzi wa jengo hilo ni sehemu ya huduma za kijamii zinazoilenga sekta ya afya ambapo benki hiyo imeweka utaratibu wa kusaidia.
Alisema kukamilika kwa jengo hilo la kupumzikia kutasaidia wagonjwa wa nje na ndugu zao ambao hufika kupata huduma JKCI kupumzika sehemu tulivu na salama huku wakisubiri kuhudumiwa na madaktari wa kituo hicho bila kero. Alisema msaada huo NMB inaamini imeutoa kwa wateja wao pia ambao nao hufika na kupata huduma katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kukamilika kwa jengo hilo la kusubiria pia itatoa fursa kwa madaktari kuwahudumia wagonjwa wao kwa ufasaha zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na wanahabari kabla ya kuzinduwa jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao wanaokwenda kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kuzinduwa jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao wanaokwenda kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi akifuatilia mazungumzo hayo.
Aidha, Bi. Bussemaker aliongeza kuwa Benki ya NMB kwa mwaka 2017 imepanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni moja kusaidia huduma za kijamii hususani katika sekta ya afya, elimu pamoja na kusaidia majanga mengine yanayoikumba jamii. Kwa mwaka 2016 benki hiyo ilitumia takribani milioni 260 nchi nzima kusaidia vifaa mbalimbali vya hospitalini huku jumla ya hospitali 33 zikinufaika kwa msaada huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi aliishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo na kudai hii sio mara ya kwanza kwa benki hiyo kuisaidia JKCI katika shughuli zake. Alimpongeza msaada huo ni mkubwa kwao na unajenga mazingira mazuri ya huduma kwa wateja wao hivyo kuishukuru sana NMB pamoja na uongozi na wafanyakazi wake.

No comments: