Advertisements

Saturday, May 6, 2017

DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAHIMIZA WANAFUNZI KUSOMA VITABU

Wananafunzi wa Shule za Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada na ziada, ili waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi, alipozungumza na wanafunzi, walimu na wajumbe ya Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho, wakati akizindua maktaba iliyokarabatiwa na mfuko huo. Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya msingi Makumbusho jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz)

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana mwalimu mmoja akasomeshwe taaluma hiyo. Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akizungumza alipokuwa akimkaribisha Mama Jacqueline Mengi.



Aidha Mama Jaqueline Mengi amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi za msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu. Shule ya Msingi Makumbusho inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya kwanza katika kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada wa vitabu na Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi Hananasifu.  
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi alipowasili katika shule ya msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi. Katikati ni Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni katika uzinduzi huo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyekwamilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni. Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule msingi Makumbusho kabla ya uzinduzi huo. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimwongoza Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi kuelekea eneo la uzinduzi wa maktaba hiyo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la maktaba hiyo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akisoma moja ya vitabu vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni kwa pamoja wakizundua rasmi eneo la kuhifadhia vitabu ndani ya maktaba hiyo. Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim (wa pili kulia). Baadhi ya watoto wa shule ya msingi Makumbusho wakisoma vitabu mbalimbali vilivyotolewa msaada na Dr. Ntuyabaliwe Foundation. Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule wakikagua vitabu katika maktaba hiyo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha na walimu pamoja na wajumbe wa kamati shule. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowakilisha wenzao. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo (katikati) akionyesha waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) muonekano wa awali kabla ya jengo hilo kukarabatiwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation. Kushoto ni Mama Mengi na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Shule, Haji Shabani Kibwana. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akifurahi na kuimba na wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho baada ya kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi wa maktaba shuleni hapo.

No comments: