Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUP)
Dkt.Stephen Nindi akizungumza kwa ufupi hatua iliyofika kabla ya kwenda kukabidhi rasimu hiyo katika vyombo vya juu
Mkurugenzi msaidizi nyanda za malisho kutoka wizara ya kilimo na Mifugo Bw. Victor Mwita(Kulia) ambaye alikuwa mwenyekiti wakati wa shughuli hiyo, akitoa mwongozo wa baadhi ya mambo.
Baadhi ya watumishi Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUP) wakiwa wanafuatilia kwa makini majadiliano hayo wakiwa mkoani Morogoro.
Mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho akichangia jambo wakati wa mjadala
Bi. Amina Ndiko kutoka Shirika la kimataifa la Oxfam nchini Tanzania akitoa neno la shukurani mara baada ya kukamilisha zoezi la kukamilisha mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi.
Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care Bi. Mary Ndaro akizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo changamoto kubwa iliyopo inayochangia ucheleweshaji wa upimaji wa ardhi ni pamoja na kuwepo kwa bajeti ndogo
Bw. Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Idara ya Misitu na Nyuki akichangia jambo wakati wa kukamilisha mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi
Kikosi kazi wakiendelea na kazi ya majumuisho
Bw. Zakaria Faustin Mratibu wa kitengo cha Ardhi na uwekezaji kutoka (TNRF) akizungumza jambo wakati wa majumuisho hayo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikosi kazi
Kikosi Kazi cha Masuala ya Matumizi ya Ardhi
kinachojumuisha wadau kutoka serikalini na asasi za kiraia wamekutana na
kukamilisha rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya ardhi
nchini. Mkakati itakayowasilishwa katika ngazi ya juu endapo utatekelezwa ,kusimamiwa na kufatiliwa kwa umakini kwa asilimia kubwa nchi ya
Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zenye utulivu wa migogoro ya ardhi
Miongoni mwa wadau hao waliohudhuria katika kikao wapo kutoka
taasisi za serikali na zisizo za serikali ikiwemo Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya
Ardhi(NLUP),Shirika la kimataifa la Care pamoja Shirika la Oxfam.
Akizungumza Mkoani
Morogoro ,Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUP)
Dkt.Stephen Nindi alisema endapo rasimu
hiyo itapitishwa na yale yaliyokuwepo ndani ya rasimu yakasimamiwa na kufatiliwa vizuri kwa kiasi kikubwa
itawezesha vijiji na Wilaya kuwa na mpango mzuri wa matumizi bora
ya Ardhi.
“Ndani ya rasimu hiyo imeweza kuchambua vizuri suala zima la
matumizi ya Ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa itaondoa na kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi katika maeneo
mengi ya nchi, baada ya rasimu hiyo kukamilika itaweza kupelekwa katika ngazi
ya juu kwa ajili ya kupewa baraka na kuanza
utekelezaji wake.” Alisema Dkt. Nindi
Alisema kuwa kikosi kazi hicho kimeweza kutengeneza mipango
ya ardhi takribani 100 kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kikosi kazi hicho
kipipo undwa.
"Ile kazi ambayo tuliifanya kipindi kirefu kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka Serikali na taasisi zisizo za kiserikali
tangu mwaka jana kwa sasa imefikia katika hatua ya mwisho ya kuwasilishwa katika vyombo vya juu kwa lengo
la kupewa baraka ili utekelezaji wa
jambo hilo
liweze kuanza ,"alisema Dkt Nindi
Nae Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care Bi. Mary Ndaro alisema kuwa lengo kubwa la wao kukutana na wadau mbalimbali wa mipango ya matumizi bora ya ardhi ni pamoja na kuhakikisha kuwa kuna kasi ya upangaji wa ardhi katika nchi.
"Moja ya changamoto kubwa iliyopo inayochangia
ucheleweshaji wa upimaji wa ardhi ni pamoja na kuwepo kwa bajeti ndogo.Maeneo mengi yakipimwa yanasaidia kuwepo kwa usalama wa
miliki na hati miliki hususani kwa wananchi wa vijijini ambapo karibia asilimia 60 ya wananchi
wanategemea ardhi kwa ajili ya kujipatia kipato hivyo kama nchi ni vema
kuwekeza katika upangaji wa matumizi ya ardhi ili kusaidia kupunguza migogoro
ya ardhi,”alisema Ndaro
No comments:
Post a Comment