Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala, akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Kundemba FC,Mohamed Haji Shaibu, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Masauni - Jazeera Cup.Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani.Mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Visiwani Zanzibar. Picha na Abubakari Akida
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdulla Juma Saadala, akimkabidhi zawadi ya viatu mchezaji bora wa mashindano ya Masauni - Jazeerah Cup,Shabani Makuka.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC kuibuka mshindi dhidi ya Kilimani Maghorofani, mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmmoja,Visiwani Zanzibar
Mwamuzi Bora wa Mashindano ya Masauni - Jazeera Cup, Ramadhani Khamis Kombo akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala,b aada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali kati ya timu ya Kundemba FC na Kilimani Maghorofani.Mchezo huo ulifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Visiwani Zanzibar.
Nahodha wa timu ya Kundemba FC, Mohamed Haji Shaibu, akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya Masauni-Jazeera Cup kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt.Abdulla Juma Saadala.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni
Nahodha wa timu ya Kundemba FC,Mohamed Haji Shaibu, akifurahia fedha za zawadi ya mshindi wa kwanza mashindano ya Masauni-Jazeera baada ya kuzipokea kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala,(aliyeshika kombe)
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala, akizungumza na wananchi (hawapo pichani), waliofika kuangalia mchezo wa fainali wa mashindano ya Masauni - Jazeera Cup.Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani,uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmmoja, Visiwani Zanzibar.
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Dkt.Abdulla Juma Saadala, akizungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo wa fainali wa mashindano ya Masauni - Jazeera Cup. Wapili kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni,Nassor Saleh Jazeera na wanne ni Mbunge wa jimbo hilo Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Visiwani Zanzibar.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Kundemba FC, wakishangilia kuibuka mabingwa wa mashindano ya Masauni - Jazeera Cup, baada ya kuifunga timu ya Kilimani Maghorofani kwa ushindi wa mikwaju ya penati 8-7.Mchezo huo ulifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Visiwani Zanzibar
No comments:
Post a Comment