Rais John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha kutengeneza dawa za kuulia vimelea vya mbu wanaosababisha malaria kilichopo Kibaha, Pwani.
Magufuli amevamia katika kiwanda hicho leo (Alhamisi) katika siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Pwani na kuzipa siku 10 halmashauri, manispaa na majiji nchini kwenda kuchukua dawa hizo za kuua vijidudu vya malaria na kuzipulizia katika maeneo yao yalipo makazi ya watu.
“Sasa mimi nimeshatoa agizo dawa zilipiwe, sasa nione mkurugenzi ambaye atashindwa kutekeleza agizo langu la kufata dawa hizo kwa kipindi nilichotoa, nimesema natoa muda mpaka mwisho wa mwezi, "amesema Rais Magufuli.
Kadhalika, Rais ameiagiza Wizara ya Fedha kutoa Sh1.3 bilioni kwa ajili ya kulipia lita 100 ya dawa hizo za kuua vimelea vya mbu zilizopo katika kiwanda hicho.
Kadhalika, Mziray amefafanua zaidi na kumweleza Rais kuwa kushindikana kununuliwa dawa hizo kwa wakati kunaweza kusababisha zikaharibika kwa sababu zinatakiwa zisihifadhiwe zaidi ya miezi miwili tangu zinapotengenezwa.
No comments:
Post a Comment