Floyd Mayweather Jr amsukumia ngumi maridadi ya mkono wa kulia Conor McGregor
Mchuano mkali wa ndondi kati ya Conor McGregor na mwanandondi Floyd Mayweather Jr umemalizika huko Las Vegas, Nevada nchini Marekani, baada ya kuchelewa kuanza kwa muda wa saa moja hivi.
Bondia Floyd Mayweather Jnr, akimlemea Conor McGregor kwa makonde mazito mazito kabla ya kumalizika raundi ya 10.
Masumbwi hayo yalikuwa ya raundi kumi. Awali wachanganuzi walisema kuwa Floyd Mayweather Jnr alikuwa ameanza kulemewa katika raundi tatu za mwanzo na mpinzani wake, kabla ya kujizoazoa na kuanza kumrushia makonde mazito mazito Conor McGregor, ambaye alionekana kulemewa hasa kuanzia raundi ya saba.
Maelfu ya watu wamefika katika mji wa Las Vegas katika jimbo la Nevada nchini Marekani, kutizama mchuano huo mkali wa ndondi, unaofanyika leo Jumapili.
Conor McGregor akimtupia konde Floyd Mayweather Jnr
Alishindwa kuhimili makonde mazito ya Maywheather na kushindwa kumaliza raundi ya 10.
Tayari McGregor ambaye amechana chale mwilini, ni bingwa wa taji la Ultimate Fighting- mchezo ambao mwanandondi anatumia mbinu zote za upiganaji, akitumia makonde na mateke.
Lakini nyota huyo wa miaka 29, hawajawahi kushiriki mchuano wa makonde ya kulipwa- Huku May-weather menye umri wa miaka 40 akitajwa kuwa mpinzani wake hatari zaidi katika masumbwi.
Dola milioni 600 zinatazamiwa kupatikana kutokana na mauzo ya moja kwa moja ya tiketi ya kutizama makabiliano hayo ya ndondi. Ambayo pia inatizamwa na mamilioni ya watu moja kwa moja kwenye Runinga huku wengine wengi wakifuatilia katika mitandao.
Floyd Mayweather mara tu baada ya kushinda
Pambano la Money Fight baina ya
bondia Floyd Mayweather na Conor McGregor limeweka historia ya
kuwavutia nyota kibao waliohudhuria.
Miongoni mwa nyota walioshuhudia
Maywether Jr akiibuka na ushindi ni pamoja na Leonardo Di Caprio,
Bruce Willis, Demi Lovato, Mike Tyson na LeBron James.
Mkali wa filamu muingizaji wa picha kama Die Hard, Bruce Willis akifuatilia pambano hilo
Mwanamuziki Demi Lavota akiimba wimbo wa taifa kabla ya pambano hilo
Mchezaji nyota wa kikapu LeBron James naye hakutaka kupitwa na pambano la Money Fight
Ozzy, Sharon pamoja na Jack Osbourne nao walikuwapo kushuhudia pambano hilo
No comments:
Post a Comment