Advertisements

Sunday, August 13, 2017

RAIS MAGUFULI NA MKEWE WAUNGANA NA WAUMINI MISA TAKATIFU KANISA LA ST. JOSEPH

Rais Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wakagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2017.
Rais Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wakitakiana amani na watawa wakati wa Ibada ya Misa hiyo.
Rais Magufuli akiwapungia mkono waumini baada ya kushiriki Ibada ya Misa.
Rais Magufuli akipiga picha ya kumbukumbu na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Padre Vicent na baadhi ya wanafunzi shule ya Sekondari ya St. Joseph baada ya kushiriki Ibada ya Misa hiyo.
…Wakijumuika na waumini wengine kushiriki Ibada ya Misa hiyo.
Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Misa takatifu.

No comments: