Dar es Salaam. Wahamiaji haramu wanane kutoka Ethiopia wamekamatwa wakisafirishwa kwa lori la kampuni ya Dangote kwenda Mtwara.
Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Edward Chegero amesema leo Alhamisi kuwa, wahamiaji hao walikamatwa Kongowe wilayani Temeke.
Amesema wamekamatwa jana Jumatano baada ya idara kupata taarifa na baadaye kuweka mtego uliowanasa.
Chegero amesema mbali na wahamiaji hao, idara imewakamata Watanzania wanne waliokuwa wakiwasindikiza wahamiaji hao.
Amesema Watanzania hao walikuwa wakitumia gari aina ya Toyota Passo.
Kaimu kamishna amesema uchunguzi unaendelea ili kuwakamata wahusika wote wa mtandao huo.
Chegero amesema baadhi ya wahamiaji hao walikuwa na tiketi zinazoonyesha wanatoka Msatakwenda Dar es Salaam.
Amewataka madereva wa malori na usafiri mwingine kutosafirisha wahamiaji haramu kwa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja cha sheria.
Kaimu kamishna pia amewaonya wamiliki wa nyumba za wageni zinazotumika kuwaficha wahamiaji hao akisema kiama kwao kinakuja.
No comments:
Post a Comment