ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 10, 2017

MAONI BINAFSI, KUKUA KWA SOKA TANZANIA.

Related image
Ili mpira wetu ukue, lazima tubinafsishe Club zetu. Zimilikiwe na makampuni au watu binafsi. Ubinafsishaji wa vilabu ni salama kwa wanaoiunga mkono klabu husika na ni salama zaidi wa wadhamini(Makampuni) yanayoyaka kuwekeza kwenye mpira... Mbali zaidi kubinafsisha mpita ni MASTER KEY ya kukuza soka letu kuanzia vipato vya wachezaji, club na hata timu ya Taifa.

Hizi mambo za kukaa kwenye bao, sijui wazee wa club.. wanachama n. k havitupeleki popote, miaka kadhaaa mifumo yunayotumia kuendeshea SOKA LETU imegubikwa na USINGIZI FOFO usioleta mabadiliko yoyote yale kitaifa na hata tunalokwenda kimataifa.

My Dream ni kuona tunaondoa vilabu vyetu kutoka Community based Clubs to Company/personal owned Clubs.

Leo Simba inauzwa... Naunga Mkono transformation hii, na sio siku nyingi Simba itakuwa level nyingine.

Sisi Singida United kwa muda mfupi tuliojiendesha tumeona mafanikio, lakini tungekuwa kwenye lilekundi la.. wazee sijui wanachama.. sijui n. k tusingefika hapa.

Wadhamini unapo waaproach kuomba udhamini moja ya swali lao ni mfumo wa uendeshaji wa Club yako. Wakiona ni Community based Club yaani Club hainamwenyewe wanakwepa.. kwa sababu wanaogopa kuwekeza pesa zao kwa management inayoweza kupinduliwa muda wowote.

Hivyo acha tu ruhusu uwekezaji binafsi kwenye mpira, pesa zifanyekazi yake kukuza soka letu.

Samahani sijachimbua kiundani zaidi na hata kuonesha mifano hai ya nchi ambazo tunatamani tuwe kama wao jinsi mifumo ya kuendesha soka kikampuni au umiliki binafsi linavyoleta matokeo Chanya.

Sambamba na hilo PITCH za nchi yetu ni dukuduku ninaloliangalia kivingine, tunakazi ya kufanya kuanzia serikali, wamiliki wa viwanja, wadau wa mpira(wadhamini), na sisi vilabu vya mpira wa miguu.
By. Festo Sanga
Mkurugenzi Singida United Fc

10/10/2017

No comments: