Mmoja kati ya kundi kubwa la ng’ombe akishushwa baada ya kuwasili katika eneo la kuchinja mapema leo tayari kwa kuchinjwa. Waislamu duniani kote wanasherehekea sikukuu ya Idi ambayo husherehekewa kwa kutoa sadaka ya kuchinja. Ngombe takriban 600 wanatarajiwa kuchinjwa katika kipindi cha siku nne.
Kundi la ng’ombe wakiwa wamelazwa chini tayari kwa kuchinjwa katika sikukuu ya Idi inayosherehekewa duniani kote na waumini wa dini ya Kiislamu, siku hii ni siku maalumu ya kuchinja na kutoa sadaka. Ng’ombe zaidi ya 600 watachinjwa mpaka kufikia kilele cha maadhimisho ya sikukuu hiyo. Tukio la kuchinja limefanyika jijini Dar es Salaam katika shule ya Feza Boys iliyoko Kunduchi.
Tukio la kuchinja likiambatana na dua linaendelea
Waandaaji wa nyama iliyochinjwa katika siku ya kuchinja ambayo ni sikukuu ya Idi ambayo pia huambatana na hija. Waislamu duniani kote leo wanasherehekea Sikukuu ya Idi.
Wasimamizi wa kugawa nyama iliyojinjwa kama sadaka leo katika kituo cha shule ya Feza Boys iliyoko Kunduchi, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Tukio hilo hufanyika kila mwaka katika kuadhimisha sikukuu ya Idi. Ng’ombe hukusanywa kutoka kwa wafugaji mbalimbali nchini kwaajili ya kukamilisha tukio la kuchinja ili kutoa sadaka.
PICHA ZOTE NA BLOG YA IMMA MATUKIO
No comments:
Post a Comment