ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 16, 2017

NAIBU WAZIRI NISHATI AWASILI MAKAO MAKUU YA WIZARA DODOMA

Na Veronica Simba – Dodoma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Khamis Mgalu, ameripoti rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma asubuhi hii, Oktoba 16, 2017.
Naibu Waziri Mgalu amepokelewa na watumishi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini waliopo Dodoma, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda.
Baada ya kuwasili, Naibu Waziri ametumia muda mfupi kuzungumza na wafanyakazi ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma.
Akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya wafanyakazi, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Miriam Mbaga, amemwahidi Naibu Waziri kuwa, wafanyakazi wako tayari kumpa ushirikiano yeye na viongozi wengine wa Wizara ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwatumikia wananchi kikamlifu.
Naibu Waziri Mgalu, ni miongoni mwa Mawaziri wapya walioteuliwa na Rais John Magufuli na kuapishwa Oktoba 9, 2017, wakati alipofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda (kulia), akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Subira Mgalu, Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani), aliporipoti rasmi Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Miriam Mbaga, akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, wakati wakimpokea Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani).
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akizungumza na wafanyakazi aliporipoti rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Amon Marco (wa pili kutoka kulia), akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), wakati Naibu Waziri alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akisalimiana na watumishi, alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

No comments: