Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kulia) hii leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad (katikati) Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuendelea kushirikiana katika sekta ya Hifadhi na Usimamizi endelevu wa mazingira nchini.
Sehemu ya wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na wale wa Ubalozi wa Norway wakifuatilia majadiliano hayo baina ya Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Makamba akiongea na wageni kutoka Ubalozi wa Norway hapa nchini walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment