ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 27, 2017

SHIRIKA LA HAKI ELIMU YASHIRIKIANA NA JAMII KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU.


Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Haki Elimu nchini John Kalage akipanda mti katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na
wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu jana (Habari, Picha na  Pamela Mollel, Arusha)

Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wao John Kalage wa tatu kushoto, wakichimba shimo kwaajili ya kuhifadhi taka ngumu katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii

Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakijiandaa kwenda kupaka rangi madarasa katikashule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Haki Elimu nchini John Kalage akipongezwa na Mkuu wa shule hiyo Vitalis Nada mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika shule hiyo jana
Mmoja wa wazazi shuleni hapo akishiriki zoezi la umwagiliaji wa maua katka maadhimisho ya huduma kwa jamii iliyoratibiwa na Shirika na Haki Elimu
Wafanyakazi wa Haki Elimu wakiwa wananendelea na zoezi la upakaji rangi shule hapo jana
Aliyeshika ndoo nyekundu ni Abraham Lazaro kutoka Idara ya Habari na uchechemuzi akiwa na mfanyakazi mwenzake wakiendelea na zoezi la umwagiliaji katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii

Mwanafunzi shuleni hapo akiwa amebeba ndoo kwaajili ya kubebea maji kwaajili ya shughuli yaumwagiliaji shuleni hapo jana
Meneja Idaraya Huduma, fedha na Utawala Daniel Luhamo akichimba shimo la kuhifadhia takangumu shuleni hapo
Mfanyakazi wa Haki Elimu Raphael akiendelee na shughuli ya upakaji rangi
RoseMwenda Mmoja wa wafanyakazi wa HakiElimu kutoka Idara ya Ushiriki naUwajibikaji wa jamii akipaka rangi bati katika shule ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha


Mwanafunziwa kidato cha nne shule ya Sekondari MukulatStella Massawe akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa HakiElimu John Kalage,zawadi iliyotengeneza katika klabu yaoya wanafunzi ya Njoo Tuzungumze
Mkuu wa Miradi HakiElimu – Boniventura Godfrey akibeba ndoo za kuchotea maji kwaajili bya umwagiliaji
Baadhi ya wazazi wakisalimia katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na tunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu
Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri akimkabidhi zawadi iliyotolewa na bodi ya shule kwa Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini John Kalage kwa kutambua umuhimu wa elimu Nchini
                                                                                                                   Picha ya pamoja 

Na Pamela Mollel,Arusha


Shirika lisilo la kiserikali nchini Haki Elimu limetoa shilingi milioni ishirini ya kuanzishwa kwa ujenzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari mukulat katika kijiji cha lemanyata kata ya lemanyata wilaya ya arusha vijijini ili kuwaondolea adha wanafunzi i wa shule hiyo wanaolazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia muda mwingi kwakutafuta maji.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat Mkurugenzi wa haki elimu nchini john kalaghe amesema shirika la haki elimu limeamua kushirikiana na jamii katika kuondoa changamoto katka sekta ya elimu katika shule hiyo ikiwamo tatitzo la maji pamoja na kuboresha mazingira kwa kupanda miti pamoja na kukarabati majedarasa hayo kwa kupiga rangi.

Shirika hilo la haki elimu kwa kupitia kwa mkurugenzi huyo wameahidi kutoa ufadhi kwa kuwalipia karo wanafunzi wa shule ya sekondani ya mukulat watakaofanya vizuri kwa ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihni hasa kwa mtoto wa kike ambaye anaonekana yuko nyuma kwa mambo ya elimu hasa katika jamii ya
kifugaji.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaa ya Arusha vijijini katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii ,afisa elimu wa wilaya hiyo B akari kimath amelipongeza shirika la haki elimu kwa kuanzisha mradi wa maji katika shule hiyo pamoja na upandaji wa miti na ukarabati wa madarasa na amesema miradi hiyo itapunguza changamoto za elimu zinazozikabili shule za msingi na sekndari wilayani humo na kuliomba shirika hilo kuendela na msaada huo katika shule zilizoko pembezoni mwa wilaya ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora

Ameiomba jamii kushirikiana na mashirika yasyoyakiserikali kupungumza changamoto yanaozikabili shule za msingi na sekondari na kuitaka jamii kuhakikisha wanatunza miradi hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi
walikuwa wanapata shida kwa usafuri umbali mrefu kutafuta maji.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha miradi shirika la haki elimu Boniventura Godfrey amesema kwa kutambua changamoto zinazoikabili
sekta ya elimu nchni tayari wameanzisha mpango maalumu wa kuzisaidia shule za msingi na sekondari 127 katika wilaya ishirini na mbili kwa kuwasaidia miradi ya maji,uwekaji wa umeme wa jua ,ukarabati wa madarsa,na upelekaji wa vifaa vya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu katika mzngira bora.

Awali wakizungumzi miradi hiyo wanafunzi wa shule ya sekondari Mukulat Stella Massawe wamelishukuru shirika la haki elimu kwa uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo kwa kuwa mradi huo wa maji utawapungumzia changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa kusafuri umbali mrefu kwa kutafuta maji pamoj na kutumia muda wa masomo hivyo ,kupungua kwa changamoto hizo kutapunguza suala la utoro kwa wanafunzi.

No comments: