Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa vituo vya hali ya hewa vilivyofungwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya usimamizi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ambapo kutokana na uwezo wa vituo hivyo taarifa zake zinatumika kutabiri uwepo maafa ya mafuriko na Ukame nchini, kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya, Meneja Kanda ya Kusini, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Daudi Amas na Mratibu Mradi wa mifumo ya Tahadhari za mapema, Alfei Daniel, wakati alipokuwa anakagua vituo hivyo mkoani Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, David CChilambo, juu ya jinsi vituo vya hali ya hewa vilivyofungwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya usimamizi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ambapo kutokana na uwezo wa vituo hivyo taarifa zake zinatumika kutabiri uwepo maafa ya mafuriko na Ukame nchini, , wakati alipokuwa anakagua vituo hivyo mkoani Ruvuma, katikati ni Mkuu wa Wilaya Namtumbo, Luckness Amlima.
Moja ya Kituo cha hali ya hewa kati ya vituo 36 vilivyofungwa na Ofisi ya Waziri Mkuu nchi nzima kwa usimamizi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ambapo kutokana na uwezo wa vituo hivyo taarifa zake zinatumika kutabiri uwepo maafa ya mafuriko na Ukame nchini, , kutokana na uwezo wa vituo hivyo vinavyopatikana hapa nchini na Ethiopia kwa bara la Afrika, vimeongeza uwezo wa ufanisi wa utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kutoka asilimia 82 hadi asilimia 87 kwa sasa.
1 comment:
Taarifa haielezi sababu za kufungwa kwa vituo hivyo badala yake tunaelezwa faida iletwayo na vituo hivyo. Nimechanganyikiwa kidogo. Jee? kuna wadau wanoweza kunisaidia kutafakari hili?
Post a Comment