Advertisements

Thursday, December 28, 2017

ARUSHA WAIOMBA KAMPUNI YA ABACUS PHARMA (A) LTD KUWAPELEKEA BIDHAA ZA SUGAR FREE

Muonekano wa jiji la Arusha katika picha

Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wa jijini Arusha wameiomba Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kuwapelekea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia kupunguza  matumizi makubwa ya sukari.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo mkoani humo kusherehekea Sikukuu ya Krisimasi walisema bidhaa hizo ni mkombozi kwao.

"Binafsi napenda kusema bidhaa hizi za Sugar Free kwa hapa Arusha zitapata soko kubwa kutokana na watu wengi kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari" alisema Mzee Mollel mkazi wa Njiro.

Mollel alisema watu wengi jijini humo wananchi kwa masharti ya ulaji na unywaji wa vitu visivyo na sukari jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa karibu familia nyingi.

Alisema wakazi wa jiji hilo wamezipokea kwa mikono miwili bidhaa hizo ambapo wameiomba kampuni hizo kufungua tawi mjini humo ili bidhaa hizo ziweze kupatika wakati wote.

"Tunaomba bidhaa hizi ziuzwe na maofisa mauzo wa kampuni hiyo wasiwape wenye maduka itakuwa changamoto kupata maelezo ya kina ya matumizi yake na tunahofu wakiachiwa wafanyabiashara wengine wanaweza kutupandishia bei" alisema mkazi mwingine wa jiji hilo aliyejitambulisha kwa jina la Laizer.


Laizer alisema humo kumekuwa na unywaji na ulaji wa vyakula vyenye sukari lakini kuingia kwa bidhaa hizo zitasaidia sana wananchi hasa baada ya kupata maelekezo ya utumiaji wake.

Akizungumza bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 
Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.
"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.
Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.

Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.
Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. 
Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.

Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.
Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments: