ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 4, 2017

PONGEZI - SIMBA SPORTS CLUB NA MOHAMMED DEWJI

African Lyon FC,
PO Box 11133, 5th floor, Barclays House, 
Dar es Salaam
04/12/2017

Klabu ya African Lyon, inayocheza daraja la kwanza, inapenda kuwapongeza Sana uongozi, wanachama na washabiki wa Simba Spors Club kwa maamuzi magumu IaKini yanayobidi katika mfumo wa uendeshaji wa klabu yao. Pongezi kubwa nayo tunapenda kumpa mmiliki wetu wa zamani, Mohammed Dewji (MO) kwa kuonyesha ujasiri mkubwa katika kufanya maamuzi mazito.

Pongezi nayo lazima iende kwa SeriKali yetu ya awamu ya tano, hususan Wizara inayosimamia michezo yetu kwa kutoa mwongozo mzuri kwa vilabu vyetu, mwongozo unaoendana na uKweli wa hall ya mpira ya dunia ya leo lakini vile vile unaowalinda waanzilishi na wanachama wa vilabu vyetu.

Tasnia ya mpira ya nchi yetu ni ndogo na imekuwa haiendani kabisa na mapenzi ya watanzania waliyonayo na mchezo wa mpira. Uwekezaji wa Mohamed Dewji kwenye timu ya Simba ni ishara Kubwa na yenye uzito Kwamba ana imani kubwa na Tasnia ya mpira hapa Tanzania na yuKo tayari Kushirikiana na sisi sote kuhakikisha hii tasnia inakuwa na inashika nafasi inayostahili hapa Tanzania.

Kwetu sisi klabu ndogo, tuna imani uweKezaji wa MO utawapa moyo Sana, wadau wengineo wengi ambao wataona mwanga kwenye tasnia ya mpira na wao watafuata nyayo za MO sio katika kununua tu hisa za vilabu zingine ball kwenye maswala Vote mengineyo yanayogusua tasnia ya mpira hususan udhamini.

Tunapenda tena kuipongeza Simba Sports Club kwa hii hatua kubwa inayofungua ukurasa mpya kwenye tasnia ya mpira hapa Tanzania. Kama zilivyo tasnia zinginezo, tasnia yaKo inaKuja Kwanza halafu ushindani wa ndani unakuja baadae.

Pamoja tutajenga na Kuimarisha tasnia ya mpira hapa Tanzania.

Rahim J. Kangezij Owner-CEO
African Lyon FC w +255 784 255 614 kaneezi@email.com

No comments: