Advertisements

Monday, December 25, 2017

TANZIA: MWANDISHI WA HABARI MAYAGE S. MAYAGE AMEFARIKI DUNIA ASUBUHI HII

Mayage S.Mayage enzi za uhai wake.

Tunasikitika kuwatangazia kuwa mwenzetu Mayage S Mayage mwandishi wa habari mkongwe hapa nchini, ambaye siku chache zilizopita waandishi na wahariri walikuwa wakichangisha fedha kwa ajili ya matibabu yake, amefariki dunia leo asubuhi saa 3.
Kwa mujibu mke wa Marehemu, Bi.Digna Mayage, mwenzetu amefariki majira ya saa 3 asubuhi, leo Desemba 25, 2017, kwenye hospitali ya Misheni Mbweni alikokuwa amelazwa

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Mbweni.Tutapeana taarifa zaidi kadri tutakapozipata

Bwana alimtoa na sasa ameamua kumtwaa

Jina lake lihimidiwe

No comments: