Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga kushoto akimkabidhi unga nahodha wa timu ya African Sports ambapo kiongozi huyo alitoa mchele kg100,unga wa sembe kg 100,Ngano kg 50, maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi ,sabuni na dawa za meno |
Sehemu
ya vitu vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu |
Katibu wa Klabu ya African
Sports,Ismail Masoud katika aliyeshika funguo akizungumza mara baada ya
kupokea msaada huo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo ambao
utakuwa chachu ya timu hiyo kumaliza ligi wanayoshiriki kwa ushindi
Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti
Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy
Mwalimu,Khatibu Kilenga aliyevaa kofia kushoto akiteta jambo na
viongozi wa klabu ya African Sports mara baada ya kukabidhi msaada huo
Katibu wa Klabu ya African Sports
Ismail Mosoud kulia akimshukuru Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy
Mwalimu,Khatibu Kilenga kwa msaada waliotoa
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MBUNGE
wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na
watoto Ummy Mwalimu amekabidhi chakula na vifaa vyengine kwa ajili
ya kuisaidia timu ya African Sports ya Jijini Tanga kujikimu katika
kambi yao iliyopo maeneo ya Donge Tanga.
Msaada
huo umefika wakati muafaka ambapo timu hiyo inajiandaa kuelekea michezo
yao miwili iliyobakia ya ligi ya Taifa Daraja la Pili inayomalizika
ndani ya wiki mbili.
Miongoni
mwa vitu alivyokabidhi ni pamoja na Mchele kg 100,Unga wa ngano kg
50,Unga wa sembe kg 100,Maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia
lita 20,chumvi,sabuni na dawa za meno ambavyo vilikabidhiwa na Khatibu
Kilenga kwa niaba ya Waziri Ummy.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi kwa niaba ya Waziri Ummy ,Kilenga aliwaambia
wametakiwa heri katika michezo miwili iliyosalia kwenye michuano hiyo.
Aidha pia ni matumaini yake kwamba katika michezo hiyo timu hiyo itaweka bidii kubwa kuhakikisha inashinda .
Naye
kwa upande wake,Katibu wa timu ya African Sports,Ismail Masoud
alimshukuru Waziri Ummy kwa sapoti kubwa anayoionyesha na kwamba sasa
wachezaji wamepata hari na nguvu ya kushinda mechi mbili zilizobakia.
Alisema
mipango ya kushinda michezo hiyo iliyobakia ni mizuri ili kuhakikisha
hawashuki daraja huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia timu
hiyo kwani ni ya wananchi.
"Tanga ina enye ,na enye ni sisi,Shime wana Tanga'Tanga Kwanza.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment