Advertisements

Monday, February 12, 2018

‘Maafisa Habari, TEHAMA ni Mawakala wa Mabadiliko’

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara,Raphael Joseph Nyanda akifungua Semina kwa Maafisa hao wa Mkoa wa Mara na Arusha.
Dkt. Peter Kilima, Mkurugenzi wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3, akizungumza wakati wa Mafunzo hayo
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo anayeshghulikia Habari na picha akitoa Salama za Idara wakati wa Semina hiyo
Bibi Rebecca Kwandu, Mkuu wa Mawasiliano Serikalini kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, akitoa Malengo ya Mafunzo hayo kwa Mikoa ya Mara na Arusha.

Na. Atley Kuni OR TAMISEMI.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Joseph Nyanda amewataka Maafisa habari na TEHAMA nchini kutekeleza majukumu yao kwakuzingatia Weledi, maarifa na ubunifu kwakuwa wao ni Mawakala wa mabadiliko.

Akifungua kikao cha siku nne mkoani humo kilicho andaliwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwakushirikiana na Mradi wa uimarishaji wa mifumo ya umma PS3, na kushirikisha maafisa habari na TEHAMA kutoka mikoa ya Mara na Arusha, amewatahadharisha maafisa hao kuwa endapo watazembea kutekeleza wajibu wao wa msingi kwa weledi basi watu wengine watapotosha umma.

“Kila mmoja miongoni mwenu anayo dhamana yakutangaza mambo mazuri yanayofanywa na serikali, lakini mkikaa kimya ninyi kama sauti za taasisi zenu watu wasio wema watapotisha maudhui hayo na mwisho wa siku kuchafua taswira ya serikali” amesisitiza Nyanda.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano serikalini, Rebbeca Kwandu, akizungumza kabla yakumkaribisha Mgeni rasmi, amewataka maafisa hao kubadilika katika utendaji wao mara baada ya mafunzo ya mfumo huo juu ya uendeshaji wa tovuti.

“Mwanzoni tulipoanzisha tovuti hizi, hatukuwa na muongozo ambao ni dira ya uendeshaji lakini mara baada ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kuandaa muongozo huu kwakushirikiana na wadau wetu PS3 ni imani yangu tutabadilika” amesema Kwandu na kuongeza kuwa uwepo wa tovuti bila ya uwepo wa habari haina maana.

Akizungumza kwa niaba ya Mradi wa PS3 Mkurugenzi anayeshughulia utawala bora na Ushirikishwa wa wananchi Dkt. Peter Kilima, amekiri kuwa Maafisa habari na Maafisa TEHAMA ndio roho ya taasisi, hivyo ushirikishwa hasa kwenye vikao vya maamuzi itakuwa ni fursa kwao kuchuja na kuujuza umma mambo mazuri ya nchi.

Awali akitoa Salaam za Idara ya habari maelezo, Mkurugenzi Msaidizi wa habari na picha Thadeus Rhodney, amesema kuwa ili kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na serikali lazima maafisa habari wawe na zana (tools) za utendaji kazi na zana yenyewe katika mustakabali wa sasa kwa ngazi za Mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa ni Tovuti.

“Wafadhali PS 3 wametuwezesha kuwa na mfumo wa Government Website Fremwork (GWF) tumieni hizi tovuti kama tools ya kuujuza umma.

Ofisi Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji mifumo ya umma chini ya mradi wa PS3 wanaendesha Mafunzo ya nanna bora ya uendeshaji wa tovuti za serikali ambapo Maafisa habari pamoja na Maafisa TEHAMA wapatao 418 nchini kote watapatiwa mafunzo
Baadhi ya Wakufunzi wa mafunzo wakifatilia kwa Makini Hotuba ya Ufunguzi.
Athuman Pemba Mmoja ya Watoa mada, akiwa anaendelea na Utoaji mada mara baada ya Ufunguzi.
Mkuu wa Mawasiliano kutoka OR TAMISEMI, Bibi Rebecca Kwandu, akiteta jambo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa muda mfupi kabla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.

No comments: