Advertisements

Wednesday, February 14, 2018

SERIKALI YAPOKEA ZANA ZITAKAZOTUMIKA KUKUSANYA NA KUTOA TAARIFA ZA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI.

 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi akifungua  kikao cha makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(kulia) akimpongeza Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi (kushoto)baada ya kufungua  kikao cha makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi  kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Meneja Miradii wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bw. Grey Saga akizungumzia miradi inayofadhiliwa na Shirika hilo wakati wa  Kikao cha Makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Miradi JSI Dkt. Tulli Tuhuma akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika makabidhiano ya zana hizo katika halfa iliyofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika  Kikao cha makabidhiano ya  zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi akikata utepe kuzindua zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika hafla ya makabidhiano ya zana hizo katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14, 2017  mjini Dodoma.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi pamoja na wadau wakionesha zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika picha ya pamoja na wadau hao mara baada ya Kikao cha makabidhiano ya  zana hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017 mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Beatrice Lyimo, MAELEZO- DODOMA
Serikali imepokea zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kwa ajili ya wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii inayojumuisha kata, vijiji na mitaa.

Zana hizo zimekabidhiwa leo mjini Dodoma kwa Kamisha wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Naftal Ng’ondi na Shirika la John Snow Inc(JSI) kushirikiana na MEASURE Evaluation na PACT Tanzania kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii(CHSSP) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID).

Wakati wa makabidhiano hayo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa ni muhimu kupeana taarifa katika utekelezaji wa mipango mbalimbali iliyopo ili kuwe na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hivyo zana hizo zitasaidia katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi.

Dkt. Naftali Ng’ondi ameongeza kuwa Serikali kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi anapata huduma stahiki.

“ Zana hizi zitasadia wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii katika kuwasaidia watoto waliopo katika mazingira hatarishi” alisema Dkt. Ng’ondi.

Nae Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la John Snow Inc (JSI) Dkt. Tulli Tuhuma amesema kuwa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii unaosimamia na JSI unalengo la kuimarisha mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii.

“Zana hizi tisa ni matokeo ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani USAID na mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI na zitawasaidia wasimamizi wa mashauri ya watoto kuweka kumbukumbu na kufuatilia mashauri ya kiulinzi, ustawi wa jamii na afya katika halmashauri na kutoa huduma pamoja na rufaa kwa watoto walio katika mazingira hatarishi”alisema Dkt. Tulli.

 Aidha, Dkt. Tulli ameongeza kuwa awali kulikuwa na muingiliano wa katika utoaji wa huduma na kusababisha ugumu katika kufanya ufuatiliaji wa huduma na upatikanaji wa takwimu.

No comments: