Advertisements

Wednesday, February 14, 2018

UHAMIAJI YAANIKA WATUMISHI WALIOACHA KAZI


Idara ya Uhamiaji imewatahadharisha wananchi kuwa makini na waliokuwa watumishi wake walioacha kazi kwa sababu mbalimbali ikiwamo kufukuzwa kati ya mwaka 2016/17.
Akizungumza na gazeti hili leo Februari 14, 2018, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala amesema watumishi hao 18 baadhi yao wamekuwa wakiendelea kujinasibisha kama watumishi wa idara hiyo.
Amesema idara imewatangaza hadharani ili kuisaidia jamii kuwatambua kwamba si watumishi wao hivyo ikitokea miongoni mwao akaendelea kajitambulisha wananchi wachukue hatua ikiwamo kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Watumishi hao ni, Thobias Lyewe, Julieth Mrema, Nina Mliga, Loveness Wilson, Wilbard Ompapson, Salama Dilunga, Philberth Chaula, Mkombozi Chodri na Alfred Mrema.
Wengine ni, Imakulata Mwakatika, Ramadhan Ally, Ritha Manganga, Jovin Max, Angela Mwabwiga, Peter Bally na Elizabeth Kibinga, Veronika Mathisa na Lucy Mnyanga.
Akifafanua zaidi, Msemaji wa Uhamiaji, Ally Mtanda amesema “Kuna shida inatokea kwa watu wengi kujitambulisha kuwa wanatoka Uhamiaji. Wanakwenda viwandani na maeneo mengine kisha kuwarubuni watu na kuchukua fedha.”
“Wale kwa namna moja au nyingine walifuzwa kazi na wengine wameacha wenyewe kazi lakini wanaendelea kujitambulisha ndiyo maana tumeamua kuitoa orodha hii ili wananchi wawatambue kwamba hawa si watumishi wetu na hatutahusika kwa lolote likitokea,” amesisitiza Mtanda


No comments: